Header Ads Widget

DKT. KIMAMBO ATEULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA WADHAMINI JKCI, APONGEZWA KWA UONGOZI BORA MUHIMBILI


MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo, ni miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyozinduliwa rasmi leo na Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb).

Aidha akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mchengerwa amempongeza Dkt. Kimambo kwa uongozi madhubuti na usimamizi bora unaoendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika taasisi hiyo na kuongeza kuwa mafanikio yanayoshuhudiwa katika taasisi za afya za umma yanatokana na uongozi wenye maono, ubunifu na usimamizi makini wa rasilimali.



Mhe. Mchengerwa amebainisha kuwa kuzinduliwa kwa bodi hiyo kunakuja wakati ambapo JKCI imeanza kutekeleza mipango mikubwa ya maendeleo ikiwemo maandalizi ya huduma za upandikizaji wa moyo, upanuzi wa huduma za uchunguzi wa kisasa na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika sekta ya tiba utalii barani Afrika.

Waziri Mchengerwa amewataka wajumbe wa Bodi ya Wadhamini walioteuliwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na uzalendo ili kuhakikisha taasisi hiyo inaendelea kuwa kielelezo cha ubora katika huduma za moyo.

Bodi iliyozinduliwa inawajumbe 1. Dkt. Hassan Mshinda - Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya JKCI, wajumbe ni Balozi Mwanaidi Majaar, Prof Hussein Kassim, CPA Godfrey Kilenga, Dkt Delilah Kimambo na Prof Appolinary Kamuhabwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI