![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo |
Na. Mwandishi Wetu,
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imetangaza marufuku ya mara moja kwa dawa zote za binadamu zenye kiambato hai kinachoitwa 'Levamisole`.
Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa Juni 26, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo amebainisha kuwa, baada ya kugundua juu ya dawa hizo zinaweza kusababisha ugonjwa hatari wa ubongo unaojulikana kama 'Leukoencephalopathy'.
"Levamisole inayotumika kutibu maambukizi ya minyoo, ikiichelewa kutibiwa inaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya hadi kusababisha vifo kwa mtumiaji.
Hivyo kuanzia sasa, hakuna utengenezaji, uagizaji, usambazaji wala uuzaji wa dawa hizo nchini kwa matumizi ya binadamu." Imebainisha TMDA.
TMDA imetoa simu 14 kwa Wauzaji na wasambazaji wote kuanzia kwa tangazo hilo kwa kuziondoa dawa zote sokoni.
Aidha, Kwa Wananchi yeyote aliye na dawa hizo nyumbani anapaswa kuzikabidhi mara moja kwenye ofisi za TMDA ikiwemo kwa ofisi zilizopo: "Dodoma, Arusha, Mbeya, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro` na mikoa mingine 3.
"TMDA itaendelea kuhakikisha dawa zote zinazouzwa nchini zina ubora, usalama na ufanisi. Wananchi wametakiwa kutoa taarifa kupitia Namba ya bure 0800110084, wakibaini dawa zisizo salama sokoni".







0 Comments