Na Matukio Daima Media
BUNDI la ufisadi latua chama cha ukombozi wa Umma (CHAUMMA) baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa chama hicho kwa kauli moja kupitisha azimio la kumvua madaraka na kumsimamisha mara moja aliyekuwa Katibu Mkuu na mgombea wao wa Urais mwaka 2025, Salum Mwalimu, kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha.Mwalimu pia anadaiwa kutokuwa na uwazi kwenye mapato na matumizi ya fedha ndani ya chama, kubadilisha msimamo wa chama kwa utashi na matakwa yake binafsi, kushindwa kuheshimu uongozi pamoja na kuendesha chama mithili ya mali yake binafsi.
Uamuzi huo mgumu umefikiwa leo Jumanne, Juni 30, 2026, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni saa chache baada ya Salum Mwalimu kuandika barua ya kwenda kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mzee Hashim Rungwe, akitaka kujiweka pembeni ili kupisha uchunguzi na kumteua Benson Kigaila kukaimu nafasi hiyo.
Hata hivyo, vyanzo vya kuaminika vimeiambia Royal TV kuwa barua hiyo ya Mwalimu imetupwa kwenye pipa la taka na wajumbe, wakitaja kuwa mtuhumiwa hana mamlaka ya kikatiba ya kujipangia adhabu wala kumteua mtu wa kukaimu nafasi yake.
Hivyo kikao hicho kimeamua kumfukuza rasmi kwa kura zote za wajumbe 31 na kumpa muda wa kukabidhi mali zote za ofisi.
Jumatatu, Juni 29, 2026, Sekretarieti Kuu ya Taifa, ikiongozwa na Benson Kigaila, Edward Kinabo, Ismail Kangeta, Aisha Madoga, na Mohamed Pume, waliwasilisha "Petition" (Waraka wa kutokuwa na imani) mbele ya Kamati Kuu wakimtuhumu Mwalimu kwa kufanya ubadhirifu wa fedha, na kuendesha chama kama mali yake binafsi. Kamati Kuu iliridhia na kupeleka azimio hilo mbele ya Halmashauri Kuu.
Mapema Jumanne, Juni 30, 2026, Salum Mwalimu alimwandikia barua Hashim Rungwe akisema: "Nakuandikia barua hii... kuhusu Kamati Kuu kuunda timu ya kuchunguza yaliyosemwa... nitakuwa tayari kujibu yatakayothibitika na hata kuwajibika navyo." Aliomba kukaa nje ya ofisi na kumkaimisha Benson Kigaila.
Jumanne, Juni 30, 2026, Halmashauri Kuu iliyoketi jijini Dar es Salaam ilipokea waraka wa makatibu wa mikoa na azimio la jana, ikagomea barua ya Salum, na kupitisha rasmi azimio la kumfukuza kazi baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa.TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII
Wakati huo huo chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kupitia Kikao cha Halmashauri Kuu yake imemteua Benson Kigaila kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, akichukua nafasi ya Salum Mwalim aliyevuliwa madaraka
Taarifa iliyotufikia muda huu kutoka chanzo chetu cha kuaminika usiku huu (leo, Jumanne Juni 30.2026) imeeleza kuwa Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu wamepiga kura ya kutokuwa na amani na Salum Mwalim hivyo kuadhimia kumfukuza kwenye nafasi hiyo, na ndipo Wajumbe kwa kauli moja waliporidhia kumteua Benson Kigaila, ambaye kabla ya hapo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHAUMMA Tanzania Bara
Mapema asubuhi ya leo kabla ya maamuzi hayo ya Halmashauri Kuu, Salum Mwalim alimwandikia barua Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Hashim Rungwe kumueleza kwamba ameamua kukaa pembeni kwa muda kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazoelekezwa dhidi yake
Hata hivyo, kwa maamuzi hayo yaliyochukuliwa usiku huu na Halmashauri Kuu ni wazi kuwa chama hicho kimeamua kumtimua moja kwa moja Salum Mwalim ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2025.






0 Comments