Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yametamatika leo june 23, 2026 ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe (Mb.), alizitaka taasisi za umma kuwekeza kwa wananchi katika kutoa huduma kwa uwazi na matumizi ya teknolojia ili kuchochea uwajibikaji jumuishi kwa maendeleo endelevu.
Aidha, Prof. Shemdoe pia alizindua mifumo ya kidijitali ya Serikali ambayo ni Government Service Directory (GSD) na Mfumo wa NGAO, yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za Serikali kwa wananchi kupitia dirisha moja la kidijitali.
TANAPA ikiwa miongoni mwa taasisi za umma walitumia jukwaa hilo kutoa elimu ya uhifadhi wa maliasili, utalii na fursa za uwekezaji kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Wizara ya Maliasili na Utalii iliibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa tuzo ya umahiri katika utoaji wa huduma pamoja na mpangilio bora wa banda.











0 Comments