Header Ads Widget

WAZIRI NDEJEMBI AWASILI TANGA KWA ZIARA YA KIKAZI

 


Waziri wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi (Mb.), amewasili mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, leo tarehe 29 Juni, 2026.


Akiwa mkoani Tanga, Waziri Ndejembi atatembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwemo Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) katika eneo la Chongoleani, Tanga, unaolenga kusafirisha mafuta ghafi yaliyogunduliwa nchini Uganda kwenda kwenye masoko ya kimataifa.

Katika ziara hiyo, Waziri Ndejembi ameambatana na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI