Header Ads Widget

HIFADHI YA TAIFA ZIWA MANYARA YAUNGANA NA WADAU KUADHIMISHA SIKU YA TWIGA DUNIANI



Katika kuadhimisha Siku ya Twiga Duniani inayoadhimishwa juni 21 kila mwaka, Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara iliungana na wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii, ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Twiga (Giraffe Research Institute), mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na jamii zinazozunguka hifadhi hiyo kwa kushiriki mbio fupi na kutoa elimu ya kuwahifadhi wanyama hao wenye shingo ndefu kuliko mamalia wote wa nchi kavu na thamani kubwa katika ikolojia na utalii wa Taifa letu.

Mbio hizo zilizotaradadi kwa kubeba dhima ya *“Twiga Fun Run 2026”* zililenga kuhamasisha umuhimu wa uhifadhi wa mnyama twiga na kuongeza uelewa kwa jamii kutambua thamani ya mnyama huyo na mchango wake katika maendeleo ya Tanzania.

Mbali na mnyama huyo kuwa na mchango katika ikolojia wa kudhibiti ukuaji wa mimea kwa kula majani, machipukizi na matawi ya miti mirefu, hivyo kusaidia kudhibiti ukuaji wa mimea na kuzuia baadhi ya spishi za miti kutawala mazingira kupita kiasi. 

Pia, twiga ni miongoni mwa alama muhimu ya Taifa la Tanzania (National symbol) inayowakilisha uzuri, amani, ustahimilivu, upekee wa utajiri wa maliasili zetu na ameendelea kutumika katika matangazo, kampeni, noti za Tanzania na Shirika la Ndege la Tanzania (ATL). 

Hivyo, twiga hao wasipotunzwa na kuhifadhiwa kwa wivu mkubwa wakatoweka, athari zake hazitakuwa katika sekta ya uhifadhi na utalii pekee bali itakuwa ni kwa Taifa zima.

Siku ya Twiga Duniani iliadhimishwa jana juni 21, 2026 katika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara. Hifadhi hiyo mbali na kusifika kwa simba wanaoparamia miti pia ni eneo mjarabu kwa kuwa na spishi mbalimbali za wanyamapori, ndege wakaazi na wahamao pamoja na twiga mnyama ambaye ni mpole na asiye na mawaa.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI