Header Ads Widget

RC KHERI ATUMIA BUSARA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA MINNE KIJIJI CHA MAGUMBIKE

 

NA FRANCIS GODWIN ,MATUKIO DAIMA MEDIA IRINGA 

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa ekari 1,052 uliodumu kwa miaka minne, kati ya mwekezaji wa kigeni anayemiliki kampuni ya Premium Active Tanzania Ltd na mkazi wa Kijiji cha Magubike, Kata ya Nzihi, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mgogoro uliokuwa ulotishia usalama wa wananchi.


Mgogoro huo ulihusisha mwekezaji wa kigeni anayemiliki kampuni ya Premium Active Tanzania Ltd na Mpambe Mnyambeyu, ambaye alikuwa na madai mbalimbali ikiwemo kuzuiwa kufanya shughuli za kimila katika makaburi ya wazazi wake yaliyopo ndani ya eneo la mgogoro, hatua inayotajwa kuleta suluhu na kurejesha amani kwa pande zinazosigana.


Mkuu huyo wa Mkoa, akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alifika katika eneo la mgogoro lililopo Kijiji cha Magubike, Kata ya Nzihi, Wilaya ya Iringa, na kuitisha mkutano mkubwa wa kijiji uliowakutanisha wananchi pamoja na pande zote mbili zilizokuwa zinakinzana katika mgogoro huo, kwa lengo la kusikiliza hoja za kila upande na kufikia muafaka wa kudumu.


Kampuni ya Premium Active Tanzania Ltd inamiliki eneo hilo baada ya kuuziwa na mtu mwingine ambaye alikuwa mwekezaji kwenye eneo hilo kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2 baada ya mwekezaji huyo kukopa Benki fedha kwa kutumia hati ya eneo hilo na aliposhindwa kulipa mkopo ndipo Benki ilifikia maamuzi ya kulipiga mnada eneo hilo ambalo ndani yake lilikuwa na vitu kama makaburi ya wazazi wa Mpambe Mnyambeyu.

Hata hivyo Mpambe Mnyambeyu amepongeza mkuu wa mkoa wa Iringa kwa kufika kutatua mgogoro huo kuwa bila hivyo hali ya usalama ilikuwa shakani kwao na mwekezaji huyo .

Mwakilishi wa Kampuni ya Premium Active Tanzania Ltd  alisema uamzi wa mkuu wa mkoa watakwenda kuutekeleza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI