Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa baada ya kutunukiwa tuzo ya Taasisi iliyotangaza maeneo yake vizuri (Outstanding Destination Marketing Organization) kwenye tuzo za ACOYA – (Africa Company of the Year Awards 2026) katika halfa iliyofanyika jioni ya tarehe 12 Juni 2026 katika Ukumbi wa Superdome, Masaki jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Denis Lazaro Londo (Mb.)
Tuzo hiyo ilipokelewa na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini TANAPA, Dr. Robert Fyumagwa akiambatana na Mkuu wa Kanda ya Mashariki Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi John Nyamhanga pamoja na watumishi wengine wa TANAPA.
Aidha, Tuzo za ACOYA ni miongoni mwa tuzo zinazotambua ubora wa Taasisi, Mashirika, Viwanda na Biashara barani Afrika zinazowakutanisha Wakurugenzi Wakuu wa Mashirika (CEOs), viongozi waandamizi, wawekezaji, mabalozi, watunga sera, wajasiriamali pamoja na wadau mbalimbali kutoka sekta tofauti kwa ajili ya kutambua mafanikio, ubunifu na uongozi bora.
Utambuzi huu unaakisi mafanikio ya TANAPA katika kutangaza Hifadhi za Taifa Tanzania na maeneo ya Malikale inayoyasimamia kwa kuzingatia ubunifu, matumizi ya teknolojia na utoaji wa huduma bora kwa watalii. Juhudi hizi zimechangia kuziweka Hifadhi za Taifa Tanzania katika nafasi ya kipekee kama miongoni mwa vivutio vinavyovutia watalii kutoka Afrika na duniani kote.
#TANAPA #ACOYA2026 #DestinationTanzania #TANAPATourism #OutstandingDestinationMarketingOrg















0 Comments