Header Ads Widget

ZIMAMOTO WAPEWA MAAGIZO MAZITO

Na Matukio DaimaApp

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kufanya ukaguzi kwenye masoko endapo watabaini wafanyabiashara waliojiunganishia umeme kiholela wawachukuliwe hatua.

Agizo hilo amelitoa jijini Dar es Salaam katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Zimamoto Duniani yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila.

Amesema kuwa, kumekuwa na tabia ya wafanyabiashara kwenye maduka na masoko kujiunganishia umeme kiholela na kusababisha hitilafu ya umeme .

Katika hatua nyengine amelitama Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kushirikiana na Wakala wa barabara Mijini na Vijijini(TARURA) pamoja na shirika la ugavi wa umeme Nchini (TANESCO)katika ujenzi wa barabara na uunganishaji wa umeme ili pindi inapotokea majanga ya moto iwe rahisi kuyadhibiti.

"Hakikisheni TARURA wanapojenga barabara mshirikiane nao ili kurahisisha Miundombinu ya barabara inapitika kirahisi pindi inapotokea majanga ya moto, amesema".DC Msando.

Nakuongeza kuwa"pia TANESCO mshirikiane nao katika uunganishaji wa mifumo ya umeme kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo masoko na maduka ili kuwa na mifumo imara ya kufikika mara majanga ya moto yanapotokea.

Awali Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Kizimamoto Ilala SACF Mabusi Peter amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea kushirikiana vizuri na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa washirika wa Zimamoto, ambapo  kwasasa Jeshi hilo lina wadau wa kujitolea wapatao 75, pia klabu 50 zenye Wanachama 1000

Aidha, amesema, kuwa sasa wapo kwenye mchakato wa kufungua vituo vingine vinne vya Zimamoto katika maeneo ya Kinyerezi,Kivule,Masaki na Kigamboni.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji Tanzania na msemaji wa jeshi hilo DCP Puyo Nzalayaimisi ameishukuru Serikali kwa kulipatia magari na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuzimia mioto na kufanya Uokoaji pindi majanga yanapotokea.

"Tunashukuru sana Serikali ya Dkt.Samia Sululu Hassan kwa kuliborsha Jeshi letu kwa kutupatia vifaa vya kisasa,na sisi tunaendelea kujitoa kwa moyo  wa dhati katika kuwahudumia Wananchi"amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI