Serikali ya mkoa wa Njombe imetangaza kuanza kuchukua hatua kali kwa viongozi wanaofuja mali za vyama vya ushirika ili kutokomeza wimbi la wizi unaofanywa na baadhi ya wasio na maadili.
Katika mkutano wa Jukwaa la vyama vya ushirika mkoa wa Njombe Mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa Njombe bwana Najim Mpate wakati akifunga mkutano huo wa siku mbili amesema imefika wakati wa kushughulika na wabadhilifu wanaowarudisha nyuma wakulima.
Naye mwenyekiti wa jukwaa la vyama vya ushirika mkoa wa Njombe Nicolaus Mlimbila amesema wakulima kupitia vyama hivyo wamekuwa wakikutana na changamoto zinazowarudisha nyuma ikiwemo kupanda kwa gharama za uendeshaji zinazosababishwa na kupanda kwa mafuta kutokana na vita vya Iran.
Kwa upande wao wakulima toka vyama vya ushirika mkoani Njombe akiwemo Benedict Mwageni na Nicolina Mlowe wamekiri kuwapo kwa gharama kubwa wakati wa kusafirisha mazao yao huku wakiiomba serikali kuona namna ya kuweka ruzuku kwenye mafuta huku wakisisitizana kulima kilimo chenye tija.
Mkutano huo ni maandalizi ya kuelekea katika mkutano mkuu wa Ushirika nchini.
Naye mwenyekiti wa jukwaa la vyama vya ushirika mkoa wa Njombe Nicolaus Mlimbila amesema wakulima kupitia vyama hivyo wamekuwa wakikutana na changamoto zinazowarudisha nyuma ikiwemo kupanda kwa gharama za uendeshaji zinazosababishwa na kupanda kwa mafuta kutokana na vita vya Iran.
Kwa upande wao wakulima toka vyama vya ushirika mkoani Njombe akiwemo Benedict Mwageni na Nicolina Mlowe wamekiri kuwapo kwa gharama kubwa wakati wa kusafirisha mazao yao huku wakiiomba serikali kuona namna ya kuweka ruzuku kwenye mafuta huku wakisisitizana kulima kilimo chenye tija.

.jpeg)

0 Comments