Header Ads Widget

KUREJEA KWA HUDUMA ZA USAFIRI WA ABIRIA KWA TRENI ZA MGR KWENDA KIGOMA, MWANZA, MOSHI NA ARUSHA



Shirika la Reli Tanzania (TRC) linapenda kuujulisha umma kuwa huduma za usafiri wa abiria kwa kutumia treni za MGR kuelekea mikoa ya Kigoma, Mwanza, Moshi na Arusha zimerejea rasmi.

Katika ratiba hii mpya, kutakuwa na safari mbili kwa wiki kuelekea Mkoa wa Kigoma, zitakazofanyika siku za Jumapili na Alhamisi, safari moja kwa wiki kuelekea Mkoa wa Mwanza kila Alhamisi,  pamoja na safari moja kwa wiki kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi itafanyika kila Ijumaa.

Huduma hizi zitaanza rasmi tarehe 18 Juni, 2026 kwa ratiba ifuatayo:

Alhamisi, tarehe 18 Juni, 2026 saa 02:00 asubuhi; Treni ya Deluxe itaondoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma na Mwanza.

Ijumaa, tarehe 19 Juni, 2026 saa 08:30 mchana; Treni ya Deluxe itaondoka Dar es Salaam kuelekea Arusha kupitia Moshi.

Jumapili, tarehe 21 Juni, 2026 saa 09:30 alasiri; Treni ya Ordinary itaondoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma.

Hatua hii imelenga  kukidhi ongezeko la mahitaji ya usafiri wa abiria katika kipindi hiki.

TRC inawashauri wasafiri kukata tiketi mapema kupitia mfumo rasmi wa ukataji tiketi uliopo kwenye Stesheni zetu na kwenye mtandao ili kuepuka usumbufu

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI