Kwenye Viwanja vya Mwembetogwa leo Jumamosi Juni 13, 2026, wakati wa Mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara Bw. John Heche, Mwanachama wa Chadema na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Iringa Mjini Mch. Peter Saimon Msigwa amewaomba radhi wananchi wa Jimbo hilo kutokana na maamuzi yake ya kukikimbia Chama hicho na kutimkia Chama Cha Mapinduzi wakati wa Uchaguzi Mkuu, akisema anajutia kwa maamuzi aliyoyafanya yakitokana na ubinafsi uliomfanya kuchukua uamuzi aliouchukua hapo awali.TAZAMA VIDEO HII BOFYA LINK
"Ninyi wananchi wa Iringa ndio mlioniweka kwenye ramani ya siasa Tanzania, nimesimama mbele yenu kwa unyenyekevu mkubwa sana kuwaomba radhi. Nilikimbia vita katikati ya matatizo, sikupaswa kufanya yale maamuzi niliyoyafanya pamoja na kwamba inawezekana niliumizwa ila nilipaswa kuangalia picha kubwa ya kutetea haki za wanyonge, kuwa sauti ya wasiokuwa na sauti, sina maneno mazuri sana, naomba mniwie radhi. Hakuna maisha magumu kama kuishi kwa wakwe, nilikuwa ukweni." Amesema Mch. Msigwa.
Msigwa akirejea historia kadhaa katika Kitabu kitakatifu cha Biblia, amesema awali alijali zaidi ubinafsi "ego" yake, akiahidi kuwa sasa atakuwa kama simba aliyepoteza watoto wake katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi CCM kinang'oka madarakani













0 Comments