BERDINA MAJINGE,
MATUKIO DAIMA MEDIA,
IRINGA.WAGOMBEA 18 wamejitokeza kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Ismani, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, William Vangimembe Lukuvi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo April,18,2026 Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wilayani humo, Sure Mwasanguti, amesema kuwa kati ya waliojitokeza wanawake wawili na wanaume 16.
Alisema kuwa zoezi la kuchukua fomu lilikuwa la siku mbili ambapo lilianza Aprili 17 hadi Aprili 18, 2026 na zoezi hilo kufungwa kupisha taratibu zinazofuata.
“Kwa mujibu wa taratibu za chama, wagombea hao sasa wataendelea na hatua inayofuata ya kupigiwa kura za maoni kwenye kata zote za jimbo hilo kesho tarehe 19 katika kata 13”alisema Mwasanguti.
Aliwataja waliochukua Fomu ni pamoja na Fred Fabian Ngajiro (vunjabei),Festo Shemu Kiswaga,Asakwe Lameck Widambe,Arif Ally Abri,Eng. Sebastian Antony Kiyoyo,Tumaini Godwin Msowoya,Watende Gwerino Kiyagi.
Wengine ni Lazaro Francis Ngwira,David Evance Komba,Thobias karlo Mwilapwa,Titho Maulilyo Cholobi,Emmanuela Kaganda Mtatifikolo,Claudio Francis Nzwaga,Josephat Gwelino Msambwa,Elias Lupituko Migodela Kazikuboma,Egidy Stanslaus Mkolwe,Dr. Abdallah Suleiman Lusasi,Tedson Johansery Ngwale.
Katibu Masanguti ameongeza kuwa chama kimejiandaa kuhakikisha mchakato wa kura za maoni unafanyika kwa amani, uwazi na kufuata taratibu zote zilizowekwa na Chama Cha Mapinduzi.
Amesisitiza kuwa hatua hii ni muhimu katika kupitisha mgombea mmoja atakayewakilisha CCM katika uchaguzi mkuu ujao, na akawapongeza wanachama wote waliojiorodhesha kwa kuonesha utayari wa kuleta maendeleo katika Jimbo la Isimani.
MWISHO.






0 Comments