Header Ads Widget

SHIMO HATARI MBANGILE (DOMA) LASABABISHA AJALI BARABARANI IRINGA–MOROGORO

 


TAZAMA VIDEO YA SHIMO BOFYA LINK HII

Na Matukio Daima Media , Mvomero

WANANCHI wa eneo la Mbangile (Doma), wilayani Mvomero mkoani Morogoro, wamelalamikia kuwepo kwa shimo kubwa katikati ya barabara kuu ya Iringa–Morogoro, wakisema limekuwa chanzo cha ajali za mara kwa mara na kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara hiyo.

Fuso lililopata ajali Leo wakati likikwepa shimo 

Wakizungumza mchana wa Leo jumamosi April 17/2026 na Matukio Daima Media , baadhi ya wakazi walisema ndani ya mwezi huu wa Aprili pekee, tayari ajali zaidi ya tatu zimeripotiwa kutokea eneo hilo, zikiwemo ajali ya lori aina ya Fuso lililokuwa limebeba mizigo ya dukani, lori la mafuta lililopata ajali na kuwaka moto, pamoja na magari madogo yanayopasuka matairi yanapopita kwenye shimo hilo.


“Tumekuwa tukijitahidi kuliziba kwa njia za kienyeji, lakini kadri siku zinavyokwenda, shimo linaendelea kupanuka na kuwa hatari zaidi,” alisema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Mabaki ya lori la Mafuta lililopata ajali hivi karibuni eneo hilo

Juma Ally na Deus Sanga ni madereva wanaotumia barabara hiyo wameeleza wasiwasi wao, wakidai kuwa hali ni mbaya hasa nyakati za usiku au mvua, ambapo shimo hilo huwa halionekani kirahisi na kuongeza uwezekano wa ajali.TAZAMA VIDEO MADEREVA BOFYA LINK HII

Aidha, wananchi wameiomba Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Morogoro kuchukua hatua za haraka kurekebisha eneo hilo kabla ya kusababisha madhara makubwa zaidi.


“Shimo lipo katikati ya barabara na karibu na daraja, hali ambayo ni hatari sana. Tunaomba mamlaka husika ifike haraka iwezekanavyo,” alisema dereva mmoja wa malori anayepita mara kwa mara katika barabara hiyo.

Hadi sasa, juhudi za kuwasiliana na TANROADS mkoa wa Morogoro ili kupata ufafanuzi zaidi hazijafanikiwa na pindi meneja akipatikana tutawajuza zaidi

Ikumbukwe kuwa barabara hii ni umuhimu kwa mikoa ya nyanda za juu kusini na nchi za kusini mwa Tanzania hivyo  matengenezo ya haraka ya haraka yanahitahika eneo hilo ili kulinda maisha ya watu na mali zao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI