Header Ads Widget

TANAPA WACHANJA MBUGA KAMPENI YA VOTE NOW 2026,YAHAMASISHA TANAPA GO APP


Timu ya Dar es Salaam imeendelea na kampeni ya #VoteNow2026, kuhamasisha upigaji kura katika taasisi mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu na vyuo vya kati, taasisi za serikali na binafsi, lengo likiwa ni kuongeza ushiriki wa Watanzania kupigia kura Nchi ya Tanzania pamoja na Hifadhi za Taifa Tanzania zilizoteuliwa kwenye tuzo za “World Travel Awards - Africa 2026”

Pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa utalii endelevu nchini

Aidha, wananchi wameelimishwa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo ndani ya Hifadhi za Taifa (ikiwemo sekta za malazi, huduma za utalii na biashara zinazochochea uchumi wa Taifa), pamoja na kuhamasishwa matumizi ya TANAPA Go App kwa urahisi wa kupata taarifa, kufanya malipo na kupanga safari zao.

#VoteNow #WordtravelAwards #Tanzaniaparks #DestinationTanzania #TanapaNextLevel







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI