Msimu wa tano wa Great Ruaha Marathon (GRUMA) umezinduliwa rasmi leo, tarehe 28/04/2026 mkoani Iringa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Kheri James, katika Mkutano wa waandishi wa habari uliyowakutanisha wadau mbalimbali wa utalii, michezo na uhifadhi, ukiwa ni mwanzo wa maandalizi wa mbio hizo zitakazofanyika tarehe 4 /7/2026 ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.
Great Ruaha Marathon si mbio tu, ni uzoefu wa kipekee unaounganisha shughuli za utalii ikiwa ni pamoja na matembezi ya miguu, (walking safari), Kuvua Samaki (sport fishing), kuendesha baiskeli (cycling) kwa siku ya tarehe 3/7/2026 pamoja na mashindano ya mbio za 5KM, 10KM na 21km kwa siku ya tarehe 4/7/2026 yote yakifanyika kwenye mandhari halisi ya asili.
Hakika ni ku-vibe na kutalii!
Usipange kukosa!
Jisajili sasa :www.greatruahamarathon.co.tz
Pia unaweza jisali kupitia TANAPA GO APP!
#Utalii #GreatRuahaMarathon #TanzaniaParks #RuahaNationalPark #Kamwene #DestinationTanzania
















0 Comments