Header Ads Widget

SERIKALI YAHAMASISHA WAFANYABIASHARA ,VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MBIO ZA TULIA MARATHON



Na Matukio Daima Media App, Mbeya


SERIKALI mkoani Mbeya imewataka vijana,wajasiriamali kuchangamkia fursa za kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kupitia mbio za mashindano ya Betika Tulia Marathon 2026.

 Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Mohamed Aziz baada ya kumwakilisha Mkuu wa Mkoa  ,Beno Malisa kwenye  kwenye uzinduzi wa mbio za awali za Betika Tulia Marathon 2026 msimu 10. 

"Vijana tumieni mbio hizo kama sehemu ya fursa za kujiajiri na kujikwamua kiuchumi msikubali kuitwa kijana usiye na kazi hivyo kuweni Wazalendo kwa kuleta amani na utulivu kwa nchi ya Tanzania  badala ya kujenga chuki kwa taifa, "amesema. 

Aziz amesema  Serikali inatambua mchango mkubwa kwa vijana na ndio maana imeweka mazingira wezeshi katika vyuo mbalimbali nchini kutoa elimu bunifu na ujuzi ambao unawezeshwa kujiajiri na kujikwamua kiuchumi. 

Aziz amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Tulia kufuatia kuona umuhimu wa kuandaa mashindano hayo kila mwaka  jambo ambalo linachochea uchumi na  kuvutiwa wawekezaji na watalii.

"Tunaona namna Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust Dk Tulia Ackson alivyo weka mkazo wa kuandaa mbio hizo kila mwaka jambo ambalo linachochea fursa za kiuchumi kwa vijana kuuza bidhaa ,lakini pia uchumi wa Mkoa kutokana na kukutanishwa watu wa mataifa mbalimbali, "amesema.

 Ofisa Michezo Taasisi ya Tulia Trust, Lugano Mwangosi amesema tukio la leo ni mbio za awali kuelekea mashindano ya Tulia Marathon 2026,ambayo yataanza Aprili 15 hadi 16, mwaka huu.

Baadhi ya washiriki wa vilabu vya mbio mkoani hapa wamesema uwepo wa mashindano hayo ni fursa kubwa kwao na kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI