NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
UFUNGUZI rasmi wa kujisajili kushiriki msimu wa tano wa mbio maarufu za Great Ruaha Marathon (GRUMA) 2026 umezinduliwa kwa kishindo Jijini Dar es Salaam ambapo washiriki wanaweza kujisajili kupitia tovuti ya www.greatRuahaMarathon.co.tz.
Mbio hizo zenye mvuto mkubwa zinataraji kufanyika Julai 4/2026 ndani ya Hifadhi ya Haifa ya Ruaha ni mbio zenye hadhi ya kimataifa zinazotaraji kushirikisha wadau wengi kuliko.
Akizungumza wakati wa mkutano wa awali wa waandishi wa Habari na wadau wa mbio hizo ulioambatana na uzinduzi wa usajili wa msimu mpya wa Great Ruaha Marathon ,Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu ambae ni mlezi wa mbio hizo aliyeongozana na msaidizi wake Cosato Chumi aliwataka watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo kwani ni fursa kubwa kiuchumi.
Alisema kuwa tukio hilo linaendelea kuwa jukwaa la kipekee la kuunganisha michezo, utalii, uhifadhi wa mazingira na afya, likiwa na lengo la kuchochea utalii wa Kusini, kuhamasisha uhifadhi wa mazingira hususan vyanzo vya maji vya Mto Ruaha Mkuu, pamoja na kujenga mshikamano baina ya wananchi na wadau wa maendeleo.
Alisema mbio hizo ni chachu kubwa kiuchumi has a kwa wadau wa uwekezaji kwani serikali china ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira bora ya uwekezaji kwa kuweka miundo mbinu yake katika ubora zaidi ili kuvutia watalii wengi zaidi.
“Mbio hizi ni tukio la kipekee linalopaswa kutangazwa duniani kote kwani ni nadra sana kwa binadamu na wanyama pori kushiriki anga moja kwa amani katika mazingira ya asili.
kuwa mbio hizo ni tukio kubwa na ni jambo la kipekee linaloinua sura ya utalii nchini ,huku akiipongeza kamati ya maandalizi kwa kazi kubwa na nzuri na endelevu katika kutangaza utalii kipekee.
Msechu aliwataka Tanapa ,mashirika na taasisi zote kushiriki kwa wingi katika mbio hizo kwani mbali ya kutalii Ila zinaunga mkono kazi kubwa na jitihada zinazofanywa na Rais Dkt Samia katika kukuza utalii na kuongeza patoa la Taifa kupitia utalii.
Alieleza kuwa uzuri wa mbio hizo mbali na mbio zenyewe waandaaji wameandaa pia vivutio vingine vya kipekee vya kiutalii kama vile sport fishing, safari za picha (game drive) na matembezi ya asili.
Hata hivyo alipongeza waandaaji kwa kushirikiana vema na vyombo vyote vya habari zikiwemo vya ndani ya mkoa wa Iringa ambako tukio hilo linafanyika kuwa ni jambo jema na zuri zaidi kwani vyombo vya habari na wanahabari wa Iringa wataendelea kutangaza na kuhamasisha washiriki kwa lugha na vionjo vya Iringa zaidi.
Huku Balozi wa mbio hizo Cosato Chumi akipongeza jitihada kubwa za waandaaji wa mbio hizo na kuwaomba wananchi wote kuendelea kuhamasishana kushiriki mbio hizo.
Rais na Mkurugenzi wa SYDP, Eward Athanas Millinga alisema mwaka huu tukio hilo linataraji kuwa na washiriki wengi kuliko kutoka mataifa mbali mbali.“Great Marathon si tukio la kawaida ni sherehe ya kipekee ya utalii, mazingira na afya. Tunawakaribisha Watanzania na wageni kutoka ndani na nje ya nchi kuja kushuhudia na kushiriki katika historia ya aina yake,” alisema Kilahama.
Akifafanha kwanini Great Ruaha Marathon ni ya Kipekee, Kilahama alisema kwa kufanyika ndani ya hifadhi ya taifa, linaloifanya kuwa mojawapo ya mbio chache sana duniani zinazofanyika katikati ya pori la wanyama.
Huku dunia ikitazama Tanzania kama kitovu kipya cha mbio za mazingira, amesema Iringa inajiweka katika ramani ya dunia kama mwenyeji wa mojawapo ya matukio muhimu ya kiutalii na kimichezo.Huku wakihimiza watanzania na watu wote duniani kuthibitisha ushiriki kupitia namba ya simu +255 673 112 753 ama kupitia tovuti ya www.greatruahamarathon.co.tz. na kuwa taarifa za mbio hizo zinapatikana Kwenye pia mitandao ya Instagram na TikTok kwa jina la Great Ruaha Marathon ama kujisajili kupitia Tovuti:www.greatruahamarathon.co.tz




















0 Comments