Hali ya usalama yaimarishwa Pakistan
Wakati huo huo, polisi katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad, tayari wameanza maandalizi ya uwezekano wa ziara ya ujumbe wa kigeni, ingawa duru ya pili ya mazungumzo bado haijathibitishwa rasmi.
Idara ya usimamizi wa trafiki ya jiji hilo imetangaza kufunga vituo vyote vya usafiri mjini Islamabad na katika mji jirani wa Rawalpindi kwa muda wa siku 10, kuanzia saa 11 jioni leo hadi Aprili 26.
Huduma za usafiri wa umma kati ya Rawalpindi, Islamabad na maeneo mengine zitasitishwa. Aidha, polisi wa usafiri wa Islamabad wamepiga marufuku magari makubwa kuingia mjini kuanzia Aprili 18.
Awali leo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan ilisema kuwa hakuna tangazo rasmi kuhusu duru ya pili ya mazungumzo.





0 Comments