Header Ads Widget

AKIBA YA MAFUTA YA NDEGE ULAYA YATABIRIWA KUTOSHELEZA KWA WIKI SITA PEKEE

 

Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta ya ndege, umeathiriwa kwa zaidi ya wiki sita, hali iliyosababisha bei ya mafuta kupanda kwa kasi.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) amesema kuwa Ulaya ina akiba ya mafuta ya ndege inayotosha kwa takriban wiki sita pekee.

Shirika hilo limesema katika ripoti yake ya wiki hii kuwa mahitaji ya biashara yatafikia kiwango cha juu mwezi Juni endapo Ulaya haitafanikiwa kuchukua nafasi ya angalau nusu ya uagizaji wake wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati.

Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta ya ndege, umeathiriwa kwa zaidi ya wiki sita kutokana na hatua za Iran kujibu mashambulizi ya Marekani na Israel, hali iliyosababisha bei kupanda kwa kasi.

Mkurugenzi Mtendaji wa IEA, Fatih Birol, ameiambia AP kuwa safari za ndege huenda zikafutwa iwapo upungufu wa mafuta utaendelea.

Katika ripoti yake ya soko la mafuta, IEA imesema mafuta ya Ghuba ndio husambaza mafuta ya ndege katika masoko ya dunia. Pia imesema nchi nyingine kubwa zinazouza mafuta yaliyosafishwa kama Korea, India na China zinategemea sana mafuta ghafi kutoka Mashariki ya Kati.

Shirika hilo limesema hali hiyo imevuruga kwa kiasi kikubwa mfumo wa usambazaji wa mafuta ya anga.

Hapo awali, Ulaya ilitegemea Mashariki ya Kati kwa hadi asilimia 75 ya uagizaji wake wa mafuta. Kwa sasa, nchi za Ulaya zinatafuta wauzaji mbadala kama Marekani na Nigeria.

Amaar Khan, mkuu wa bei ya mafuta ya ndege ya Ulaya katika Argus Media, anaamini kwamba hata kama usambazaji kutoka Ghuba ukirejea hivi karibuni, bado huenda kukawa na upungufu katika wiki za mwanzo za msimu wa joto.

"Sio uhakika, lakini bado, inaonekana kuna uwezekano mkubwa sana kwamba kutakuwa na uhaba kwa kiasi fulani katika baadhi ya maeneo ya Ulaya."

"Bila shaka, eneo kama Heathrow linaweza kupewa kipaumbele kuliko viwanja vingine vidogo vya ndege, au vituo vilivyo na mahitaji kidogo. Lakini ndiyo, hata kama usambazaji huo utakuja, itachukua wiki tano hadi sita," alisema.

Mashirika ya ndege duniani yamechukua hatua za haraka kukabiliana na kupanda kwa gharama za mafuta, ambayo kwa kawaida huchangia asilimia 20 hadi 40 ya gharama za uendeshaji.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI