![]() |
| Nyasasaurus parringtoni |
Huyu ni Nyasasaurus parringtoni, anayejulikana kama "mnyama wa Ziwa Nyasa." Uvumbuzi wake umeiweka Tanzania katika mjadala wa kimataifa kuhusu ni wapi na lini dinosaria wa kwanza walionekana duniani au waliishi.
Mabaki hayo yaligunduliwa katika Bonde la Ruhuhu, kusini mwa Tanzania, karibu na Ziwa Nyasa (ndiyo maana akaitwa Nyasasaurus). Yalipatikana kwenye tabaka la miamba ya Manda, linalojulikana pia kwa lugha ya kingereza kama Manda Beds.
Aliyekusanya mabaki hayo ya kale (fossil) ni Francis Rex Parrington (mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge) mapema miaka ya 1930. Jina la pili la mnyama huyu (parringtoni) lilitolewa kwa heshima yake. Ingawa Rex Parrington aliyapata mabaki hayo, utafiti wa kwanza ulifanywa na Alan J. Charig mwaka 1956 katika andiko lake la PhD, lakini hakulichapisha rasmi wakati huo. Jina hilo lilikuja kuthibitishwa rasmi na kutambuliwa kitalaamu mwaka 2012 na timu ya wanasayansi iliyoongozwa na Profesa Sterling Nesbitt.
Katika kina cha historia ya dunia, kabla hata ardhi yetu isiwe ardhi tunayoijua leo, kulikuwa na kipindi cha ajabu kilichojulikana kama Enzi ya Mesozoic. Enzi hii, ambayo ilidumu kwa muda wa miaka milioni 186, imegawanywa katika vipindi vitatu vikubwa: Triassic, Jurassic, na Cretaceous. Ni katika kipindi cha kwanza kabisa cha enzi hii, kipindi cha Triassic, ambapo hadithi ya dinosaurs ilianza kuandikwa. Leo, tunapojikita kwenye ufahamu wetu wa dinosaur wa kale zaidi, tunapaswa kurejea nyuma hadi kipindi hiki ambapo viumbe hawa wa ajabu walipochipua kutoka kwa vizazi vyao vya awali, wakiamsha ulimwengu kwa kuonekana kwao na hatimaye kutawala sayari kwa mamia ya mamilioni ya miaka. Msingi wa hadithi hii ni kiumbe ambacho kimebadilisha kabisa mtazamo wetu wa mwanzo wa dinosaurs, nacho ni Nyasasaurus parringtoni.
Kipindi cha Triassic, kilichokuwa kinajulikana kama kipindi cha "kabla ya dinosaur," sasa kinatambulika kama enzi ya mwanzo wa dinosaur, na Nyasasaurus ndiye anayeongoza mstari huu.
ZAMANI iliaminika kuwa Dinosaria wakongwe waliishi Amerika, na umri wao ilikuwa miaka milion 232 . Hicho ni kipindi cha mwanzo cha Jurassic.
Lakini ugunduzi wa Nyasasaurus umepindua rekodi hiyo, yeye aliishi yapata miaka milioni 243 iliyopita, kipindi cha mwishoni mwa Triassic, na kumfanya kuwa Dinosaria mkongwe zaidi Duniani.
TAARIFA hii ilipotolewa mwaka 2012 iliifanya Tanzania kuwa Nchi pekee Duniani yenye mlolongo mrefe zaidi wa Dinosaria walioishi kipindi chote cha Mesozoic: (Triassic, Jurassic, Createceous), yaani kuanzia Dinosoria mkongwe zaidi duniani mwenye umbo dogo ambaye ni Nyasasaurus Paringittoni hadi jamii ya titan Dinosaria wenye maumbo makubwa kama Shingopana songwensis, Giraffetitan, Kentrosaurus, Dicraeousaurus na wengine wengi tuuu!
Hii taarifa ya uwepo wa Nyasasaurus ilivunja kabisa rekodi ya heshima ya Mikusanyo ya Dinosaria wa Amerika ya Kusini na Kaskazini ambapo awali iliaminika kuwa ndiko chimbuko la Viumbe hawa.
Heshima hiyo kubwa zaidi ilikuwa kwa vilima vya Morrison (Morrison formation) huko Marekani. Sasa heshima hiyo ilihamia Tanzania katika Bonde la Ruhuhu, miamba Manda (Manda formation) , nakumsimika rasmi mfalme wa Nyasa (Nyasasaurus) kama ndio Dinosaria mkongwe zaidi Duniani
Utafiti zaidi unaendelea, na inawezekana kwamba siku moja tutafunua mabaki zaidi ambayo yatazidi kuthibitisha na kuendeleza hadithi hii ya ajabu ya mwanzo wa dinosaurs.

.jpg)




0 Comments