Header Ads Widget

MWANDISHI WA HABARI EDITHA KARLO AFARIKI DUNIA

 


Na Fadhili Abdallah, Kigoma 

Mwandishi wa habari anayeandikia matukio Daima kutokea mkoa Kigoma Editha Karlo amefarikia dunia.


Karlo amefariki dunia nyumbani kwao wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma baada ya kuugua kwa muda mfupi akitokea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa Kigoma,  Jacob Ruvilo alisema kuwa marehemu alipatwa na mauti Jumatano mchana akiwa nyumbani kwao wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Ruvilo alisema kuwa baada ya kupokea taarifa ya msiba huo Chama cha waandishi wa habari Kigoma wamekutana kuona namna ya kushughulikia msiba huo kwani Marehemu alikuwa pia Mwanachama wa Chama hicho cha Waandishi wa habari mkoa Kigoma.

Mwenyekiti huyo wa chama cha waandishi wa habari alisema kuwa Alhamisi  uongozi wa chama hicho utakuwa na kikao cha pamoja na familia kupanga taratibu za mazishi na taarifa itatolewa.

kwa upande wake mkurugenzi wa Matukio Daima Media Francis Godwin amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Edith Karlo kuwa mbali ya kufanya kazi Matukio Daima Editha alikuwa kama Dada kutokana na urafiki aliokuwa nao .


Hata hivyo alisema ataendelea kumuenzi Marehemu wakati wote na atashiriki mazishi yake .

Editha pia  amewahi kufanya kazi pia na Kampuni ya Habari Corporation akiwa Mwakilishi wa kampuni hiyo mkoa Kigoma na Chombo cha habari cha mtandaoni Michuzi Blog.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI