Header Ads Widget

MWANDISHI NGULI WA VITABU, ABDILATIF ABDALLA AWASILI NCHINI, KUKABIDHI TUZO ZA MWALIMU NYERERE UANDISHI BUNIFU 2026


Na. Mwandishi Wetu, Dar.

MWANDISHI Nguli wa vitabu na mshairi, Bw. Abdilatif  Abdalla, ambaye ndiye mgeni rasmi katika  halfa ya Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itakayofanyika kesho, tarehe 13 Aprili 2026, amewasili nchini tayari na kueleza kuwa ni heshima kubwa kwake kupewa hadhi hiyo.

Ameyasema hayo leo,  tarehe 12 Aprili 2026, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akieleza kuwa ni heshima kubwa kwake, kama mwandishi, kutambuliwa na kupewa nafasi ya kuwepo katika tuzo hizo.

“Hii ni heshima kubwa kwangu kama mwandishi kupata hadhi hii ya kuwa mgeni rasmi katika tuzo zenye kutambua kazi ya Hayati Nyerere ya kukuza Kiswahili duniani kote” amesema Prof.Abdalla.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo, Prof. Penina Mlama ameonesha kufurahishwa  na ujio wa mgeni rasmi na kueleza kuwa, kwa waandishi bunifu nchini ni fahari kuwa na mgeni rasmi ambaye pia ni mwandishi mwenzao.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba ambayo ndiyo mratibu wa Tuzo hiyo  amewakaribisha wageni wote katika hafla hiyo inayolenga kuendeleza uandishi bunifu na kuhamasisha utamaduni wa usomaji wa vitabu nchini.

Tuzo hizo hufanyika kila mwaka  tarehe 13 Aprili kwa lengo la kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI