Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo April 17 katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera imesababisha vifo vya watoto wanne wa familia mbili tofauti katika kata ya Kibeta baada ya nyumba walipo kuwa wamelala kuangukiwa na ukuta wa nyumba zao uliopigwa na uzio wa hoteli.
Akizungumza katika eneo la tukio mrakibu mwandamizi Joseph Ngonyani kaimu Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Kagera, ameeleza kuwa mvua hiyo imesababisha uzio wa hoteli ya Parfect umeangukia nyumba mbili na kusababisha kuta za nyumba hizo kuanguka na kusababisha vifo hivyo ikiwa ni watoto watatu wa kike na mmoja wa kiume.
“waliopoteza maisha katika familia ya Mickdard Ally ambayo imepoteza watoto wawili Maniath Mickdard miaka 4, jinsia ya kike, Nuniadi Mickdard miaka 10 jinsia ya kike na famili ya Edmundi Matungwa imepoteza watoto wawili pia Elizabert Edmundi miaka 12 na Edwin Edmundi miaka 10 jinsia ya kiume”
Aidha Kamanda Ngonyani amewataka wakazi ambao wako karibu na hoteli hiyo kuhama katika makazi hayo mpaka watakapo pewa maelezo zaidi na pia amewataka wananchi kutumia wahandisi wa majengo wakati wa ujenzi ili kuepukana na madhara yanayoweza kutokea.
“jeshi la zima moto na uokoji linatoa wito wananchi kutumia wahandisi wakati wa ujenzi na pia niwashauri wananchi kuziba nyufa za nyumba zao hasa katika kipindi hiki cha mvua ili kuepukana na mathara yanayowezakutokea”
Naye kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa, Bukoba Charlse Kaigi ameeleza kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika nyumba ya kuifadhi maiti na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini kuwa uenda watoto hao walikosa hewa kufuatia kuangukiwa na ukuta.
“miili ya marehemu imeifadhiwa katika nyumba ya kuifadhi maiti, na kwa uchunguzi tuliofanya inaonyesha watoto hao wamepoteza maisha baada ya kukosa hewa maana hakuna majeraha yanayoonekana kwa macho”
Baba mzazi wa watoto wawili waliopoteza maisha Mickdard Ally amesema kuwa ameeleza kuwa alipigiwa simu na mtoto wake mkubwa majira ya saa 11 na kueleza kuwa ukuta umeangukia nyumba yao na ndugu zake wawili hawaonekani.
“niliamka kusali swala ya asubuhi nikapigiwa simu na kijana wangu wa Kibeta kuwa ukuta wa nyumba umeanguka lakini Maniath na Nuniath hawaonekani na mimi nikapanda na kukuta wameishawatoa watoto kwenye vifusi”
Katika hatua nyingine mvua hiyo imesababisha mafuriko yaliyopelekea mfugaji mmoja katika kata ya Kashai kupoteza kuku 500 walikufa kutokana banda kujaa maji.










0 Comments