Header Ads Widget

MCT YAWAAPISHA MAJAJI WA TUZO ZA EJAT 2026

Joyce Shebe akipata kiapo mbele ya Wakili Ally Kileo


Na. Matukio Daima Media, Dar.


BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limewaapisha jopo la majaji 13 watakaosimamia mchakato wa kuwapata washindi wa msimu wa 16 wa Tuzo za Umahiri wa Habari Tanzania (EJAT) mwaka huu 2026.

Uapisho huo umefanyika mapema leo Aprili 13, 2026 Jijini Dar es Salaam, ukiongozwa na Wakili Ally Kileo, ambaye aliwaapisha majaji 10, huku wengine wawili wakiapa kwa njia ya mtandao kutokea Dodoma na Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura, amesema mfumo huo mpya wa majaji ni mabadiliko makubwa kutoka kwenye tathmini za kizamani zilizokuwa zikizingatia zaidi ubora wa uandishi na uhariri pekee. 

Kwa sasa tunaenda na mfumo mpya “Uhakiki wa nyanjani” (Field verification) unaolenga kuimarisha uaminifu wa vyombo vya habari kwa jamii.

Dkt. Egbert Mkoko akipata kiapo mbele ya Wakili Ally Kileo



Jopo hilo la majaji walioteuliwa na kuapishwa ni pamoja na: Jesse Kwayu, Joyce Shebe, Beatrice Bandawe, Rashid Kejo, Dk. Egbert Mkoko, Hassan Mhelela.

Pia wapo: Absalom Kibanda, Neville Meena, Mwanzo Millinga, Sauli Gilliard, Shifaa Said Hassan, na Aisha Dachi.

Sungura amebainisha kuwa wakati mchujo wa awali wataendelea kuzingatia misingi mikuu ya uandishi wa habari ikiwamo usawa, uwiano, uwazi, na usahihi hatua ya fainali sasa itahitaji uthibitisho wa matokeo ya kazi hiyo katika jamii.

“Tunataka kujenga imani kati ya vyombo vya habari na jamii.

Kwa kusisitiza matokeo ya habari (impact), tunaonyesha thamani halisi ya uandishi wa habari na kujibu hoja za kama kweli hadhira inanufaika na kazi zinazozalishwa.” Amesema Sungura.

Aidha,  chini ya mfumo huo mpya, majaji hawatasalia ofisini kupitia nakala za magazeti au kanda za video na sauti pekee. badala yake, mara baada ya kupata kazi 10 bora zilizochujwa, MCT itawatuma majaji nyanjani kwenda kuhakiki ukweli wa madai yaliyopo kwenye habari hizo.




Beatrice Bandawe akipata kiapo mbele ya Wakili Ally Kileo





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI