Header Ads Widget

JESHI LA POLISI MWANZA WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA

Na CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA MWANZA 

MWANZA, Kuelekea sikukuu ya Pasaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeimarisha usalama kwalengo la kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani na utulivu.

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Aprili 03, 2026 na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari na kueleza kuwa katika kipindi cha mwezi machi walijikita zaidi katika kuelimisha jamii hususani katika kuzuia uhalifu na kuendelea kuwasisitiza wananchi kudumisha amani.

Mutafungwa amewataka wananchi kutii Sheria na kujiepusha na vitendo ya kialifu vitakavyowaingiza kwenye mgogoro wa kisheria.

Aidha, amesema kuwa familia zitakapolazimika kwenda kusherehekea sikukuu nje ya makazi yao zisiache nyumba bila uangalizi ili kuepusha vitendo vya kiarifu vitakavyofanyika.

"Wazazi wasiruhusu watoto kwenda katika maeneo ya burudani bila uangalizi wa watu wazima sanjari na wamiliki wa nyumba za Kilala wageni na kumbi za starehe wahakikishe wanazingatia tahadhari zote za kiusalama kulingana na masharti ya leseni zao na kusiwe na maandalizi au uendeshaji wa disko toto", amesema

Mwisho aliwataka madereva kujiepusha na mwendo Kasi nawazingatie Sheria za usalama barabarani wakati wote

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI