Header Ads Widget

DKT. KIJAJI AKUTANA NA MAAFISA NA ASKARI WA TANAPA MAKAO MAKUU ARUSHA



Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 17, Aprili 2026 amefanya kikao kazi na maafisa na askari wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Makao Makuu jijini Arusha katika ukumbi wa Phase II. 

Akizungumza na watumishi hao, Waziri alielekeza changamoto mbalimbali za kiutendaji zinazokabili shughuli za uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za taasisi zitatuliwe. Vilevile, ametoa maelekezo ya namna bora ya kushughulikia na kuzitatua changamoto hizo kwa ufanisi na kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

Kwenye kikao hicho Mhe. Dkt. Kijaji aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas na Mkurugenzi wa Wanyamapori Dkt. Alexander Lobora huku akipokelewa na mwenyeji wake Kamishna wa Uhifadhi TANAPA CPA Musa Nassoro Kuji.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI