Header Ads Widget

WAZIRI BASHIRU AAGIZA KUSIMAMISHWA NA KUHAMISHWA VITUO VYA KAZI MAAFISA UVUVI MULEBA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

 

Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera 

Waziri wa mifugo na uvuvi Balozi Dkt Bashiru Ally Kakurwa ameagiza kusimamishwa na kuhamishwa vituo vya kazi maafisa uvuvi wilayani Muleba mkoani Kagera kwa tuhuma za kupokea rushwa na kushirikiana na watu wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu.

Balozi Kakurwa ametoa maelekezo hayo March 2 mwaka huu, wakati akizindua vituo 3 vya kukusanyia maziwa kupitia mradi shirikishi ya wasindikaji  na wazalishaji maziwa mkoa wa Kagera, ambapo amesema kuwa haiwezekani serikali inatumia nguvu kubwa kukuza sekta ya uvuvi lakini kuna watu wanarudisha nyuma jitihada hizo.

"ningeshangaa sana kuona watu hawa kama bado hawajachikuliwa hatua kuna maafisa uvuvi hapa wanashirikiana na watu waofanya uvuvi harama taarifa ninayo, maafisa mifugo wanafanya vizuri ila maafisa uvuvi ziro"

Katika hatua nyingine waziri Bashiru amesisitiza ufugaji wa kisasa wa Ng'ombe ili kuzalisha kwa tija na kukuza sekta ya ufugaji nchini kupitia mazao ya Nyama na maziwa na hivyo kuchangia katika pato la taifa, lengo likiwa ni kuingiizia nchi dola billioni moja.

"tunahitaji kufuga kisasa na ufugaji huo unahitaji malisho mazuri, eneo zuri la kufugia, mbegu zuri ya Ng'ombe na matibabu ili kuweza kuwazalisha maziwa zaidi na Nyama inayohitajika nje ya nchi hasa Nyama Ng'ombe,mbuzi na Kondoo"

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafugaji mkoani Kagera Josam Ntangeki amesema sekta ya mifugo mkoani Kagera inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo miundombinu hafifu katika vitalu, uzalishaji hafifu wa maziwa na upungufu wa malisho,

"mhe waziri nishukuru kwa kututembelea kuna changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa maziwa mfano kiwanda chetu kinauwezo wa kuchakata lita elfu 20 lakini kwa sasa tunachakata lita elfu 10 kwa siku, uhaba wa malisho hasa nyakati za kiangazi"

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege, amesema hadi sasa mradi umewezesha kutolewa kwa zaidi ya Shilingi bilioni 41  kama mikopo kwa wadau katika mnyororo wa thamani wa maziwa kwa wafugaji 92,831 na ununuzi wa mitamba 3,254 yenye thamani ya Shilingi bilioni 10.8 kwa lengo la kuongeza uzalishaji.

"mhe waziri kupitia mradi wafugaji 92,831 wamenufaika kupitia huduma za kifedha pamoja na ugani na jumla ya shilingi billioni 41 zimetolewa kama mkopo wa liba nafuu kwa wafugaji na pia mitamba 3,245 imetolewa kwa wafugaji ili kuongeza uzalishaji".

Pia amesema kupitia mradi huo umefadhili viwanda 15 vya usindikaji kwa shilingi bilioni 22, na kuongeza uwezo wa kitaifa wa uchakataji wa maziwa.

Naye mwakilishi wa Heifer International Mark Tsoxo amesema kwa kushirikiana na TADB wamekuwa wadau wakubwa katika kuwawezesha wakulima na wafugaji kufikiwa kwa urahisi zaidi. Ameeleza kuwa jumla ya mitaji yenye thamani ya shilingi million 282  imesambazwa katika kanda mbalimbali, na watu 42,700 wamefikiwa na programu hiyo, huku kwa mkoa wa Kagera pekee, zaidi ya watu 9,000 wamenufaika, ikiwa ng’ombe 300 wakitolewa kupitia mfumo wa “kopa ng’ombe, lipa maziwa” unaolenga kuongeza mzunguko wa manufaa kwa wanufaika wengine.

" kwa mkoa wa Kagera pekee, mheshimiwa waziri zaidi ya watu elfu 9 wamenufaika, ikiwa ng’ombe 300 wakitolewa kupitia mfumo wa kopa ng’ombe, lipa maziwa mfumo huu uwaongezea manufaa wafugaji na kukuza sekta ya mifugo"

Awali, akisoma lisala ya ushirika wa Maruku AMCOS, Dkt,Magidalena William amesema kuwa chama hicho kilianza rasmi biashara ya maziwa mwaka 2023 kikianzia na ukusanyaji wa lita 185 kwa siku, na sasa kimefikia lita 600 kwa siku zenye thamani ya takribani shilingi milioni 19 kwa mwezi. 

"tulianza rasmi biashara ya maziwa mwaka 2023 kikianzia na ukusanyaji wa lita 185 kwa siku, na sasa kimefikia lita 600 kwa siku zenye thamani ya takribani shilingi milioni 19 kwa mwezi. 

Waziri wa mifugo na uvuvi ametembelea vituo vya Maruku halmashauri ya Bukoba, Nshamba wilayani Muleba na Kayanga wilayani Karagwe ambapo watu 734 wamenufaika na mkopo wa zaidi ya shilingi million 200, na mitamba 139.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI