Header Ads Widget

EXPERIENCE THE WONDERS INAANZIA GETI LA NGORONGORO KUELEKEA BUSTANI YA EDEN

 


Wadigo wana msemo usemao " _baraka hubarikiwa waliobarikiwa hata kama si majaaliwa"_ Naam, ukisikia Ngorongoro ni eneo pekee unaloweza kuona Wanyama wakubwa watano (The Big 5) si hadithi za kusadikika wala Ndoto za alinacha, ni dhahiri inayothibitishwa na nuru ya upeo wa macho yako

Fikiria unaingia tu getini, umbali wa nusu kilomita upande wako wa kushoto unashuhudia mti mkubwa umepambwa na mnyama  adimu sana kuonekana nyakati za mchana, huyu si mwingine ni Anko Chui.

Sasa wakati Unamshangaa Chui inakulazimu ukimbizane na muda maana _Big Five_ wengine kama Simba, Tembo, Faru na Nyati wanakusubiri Kasoko ya Ngorongoro wakiwa wamezungungukwa na makundi ya Pundamilia, swala, Pofu, viboko, Kasongo ndege aina Falamingo, Yangeyange, ndege karani na wengine wengi.

Ngorongoro ni hifadhi ya maajabu yenye Hadhi ya kimataifa, Destination ya maajabu, Bustani  ya Eden, Nyayo za Laetoli, Tamaduni hai, Bonde la Olduvai na Mazalia ya Nyumbu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI