Header Ads Widget

WAZEE WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA NA WAZEE WASIOJIWEZA


Umoja wa wazee wastaafu wanaofanya kazi katika kiwanda cha sukari cha Mkulazi mkoani Morogoro wametoa msaada wa bidhaa za  chakula na sukari ya Mkulazi kwa Kituo cha kulelea watoto yatima na Kituo cha kulelea  wazee Fungafunga Manispaa ya Morogoro

Wakiongea baada ya kukabidhi msaada huo viongozi wa umoja huo wamesema msaada huo ni hatua moja wapo ya kuonyesha wanathamini uwepo wao kwa jamii na kuthamini mazingira wanayoishi.

Umoja huo pia wamesema wametoa msaada huo ikiwa ni shukrani kwa kuaajiliwa tena na kiwanda cha sukari Mkulazi .

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo Goodluck Kway kutoka  Kiwanda cha Sukari Mkulazi amesema Kiwanda cha Sukari Mkulazi  kitaendelea kushirikia na jamii ambayo ipo kwenye mazingira magumu .

Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo Mission to the home less children Morogoro Robart Simba amesema zawadi  na misaada inayoletwa inaongeza faraja kwa watoto.

Pia Mkurugenzi wa kituo mission to the home less children morogoro Robart simba amesema Serikaili imekua mstari wa mbale katika kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima na watoto wanaishi mazingira hatarishi huku wakishukuru zawadi zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa sikukuu mbalimbali za kidini.

Nayo wazee wanaoishi katika kituo cha kulelea wazee Fungafunga wamesema kupokea kwa msaada huo kunatoa faraja kwao.

Mwisho




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI