Header Ads Widget

TBS WAWAFIKIA WAJASIRIAMALI WANAWAKE , MAONESHO YA MIAKA 20 YA TWCC DAR ES SALAAM.

 Na Mwandishi Wetu.

Shirika la Viwango Tanzania TBS , linashiriki Maonesho ya Bidhaa za Viwanda na Biashara za Wanawake, yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam , tangu Februari 26 , na yanatarajiwa kuhitimishwa Machi , 02 , 2026 .


 
Akizungumza mapema Leo hii Machi , 01 , 2026 Meneja wa TBS Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Bi. Nuru Meghji , amesema TBS wanashiriki Maonesho hayo ya Miaka 20 ya Tanzania Women Chamber of Commerce ( TWCC ) kwa ajili ya kuwahamasisha wajasiriamali wanawake waweze kukidhi matakwa ya Viwango na kuwa na Nembo ya Ubora katika Bidhaa wanazozizalisha . 

" Tupo hapa  kwa sababu Shirika la Viwango ni wadau wakubwa wa wafanyabiashara, lakini tuko hapa kuweza  kuhamasisha wafanyabiashara waweze kukidhi Vigezo ,  Kwasabbu TBS huwa tunafanya shughuli mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara hao wanawake na tunajua kuna wafanyabiashara wengi wanawake ambao ni wajasiriamali wadogo,  kwa kuliona hilo tuna program maalum ya kuwawezesha hao wafanyabiashara wanawake ili waweze kukidhi vigezo tunafahamu kuwa ni gharama na kuna wazalishaji wengine wadogo wanawake wanakuwa hawana uwezo wa kulipia zile gharama za kuzalisha ili kukidhi viwango basi kwa programu maalum  shirika la viwango linasimamia wazalishaji hawa bure kabisa  kuweza kufikia vigezo lakini huwa wanatakiwa kupita SIDO ,  Lengo hasa la kufika hapa ni kutaka kuwahamasisha yaani mjasiriamali yoyote hana sababu au mfanyabiashara mwanamke hana sababu ya kukosa kukidhi vigezo au viwango na kuweza kuhakikisha  wananchi wanapata bidhaa zenye ubora " alisema Bi. Meghji .





Kwa upande wake Mjasiriamali Bi . Lily Mwaigomole amesema

" Nashukuru na Nimefurahi sana kuwaona maafisa wa TBS ambao wanapita kwenye mabanda kutupa elimu ya kuhusu umuhimu wa kukidhi matakwa ya Viwango na Nembo ya Ubora ya TBS , Mimi mwenyewe bado sina nembo ya ubora lakini kutokana na elimu waliotupa naanza mchakato wa kupata Nembo ili niweze kuuza bidhaa yangu kwa upana zaidi na iwe bora zaidi " alimalizia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI