Header Ads Widget

TRUMP 'HAJAFURAHIA' ALIYETEULIWA KUWA KIONGOZI MPYA WA IRAN - FOX NEWS

 

Rais Donald Trump wa Marekani amesema "hajafurahishwa" na uteuzi wa Iran wa Mojtaba Khamenei kama kiongozi wake mkuu mpya, kulingana na kipindi cha Fox News.

Mtangazaji Brian Kilmeade amesema alizungumza na rais baada ya tangazo hilo, ambaye alimwambia: "Sijafurahia."

Kilmeade hakutoa maelezo zaidi kuhusu mazungumzo hayo na Trump bado hajatoa maoni yake hadharani.

Iran yaanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Israel na mataifa ya Kiarabu

Wakati huo huo, Bahrain inaripoti idadi kubwa zaidi ya vifo katika shambulizi moja dhidi ya nchi za Ghuba tangu vita kuanza.

Wizara yake ya Afya inasema shambulizi lililotokea nchini humo la ndege zisizo na rubani liliwajeruhi raia 32, wakiwemo watoto wanne, mdogo wao akiwa na umri wa miezi miwili.

Takriban watu 10 wameuawa kote eneo la Ghuba hadi kufikia sasa, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa usalama au wafanyakazi wa kigeni. Qatar, Kuwait, Falme za Kiarabu na Saudi Arabia pia ziliripoti mashambulizi mapya usiku kucha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI