Header Ads Widget

MURTAZA ADAMJEE : TUWAJENGEE UWEZO WA MATENDO MEMA VIJANA

Mkurugenzi wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee


Na. Mwandishi Wetu, Dar.


MKURUGENZI wa Radiant Africa Limited, Murtaza Adamjee ametoa wito kwa Jamii kuwa na misingi ya Imani kwa kufanya matendo mema hususani Vijana kwani Mungu anatoa baraka.

Murtaza ameyasema hayo katika kongamano maalum lililoandaliwa na Good Deeds Day Tanzania likiwa na lengo kuwajengea uwezo na kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa matendo mema katika kusaidia Jamii.

Ambapo amebainisha kuwa, kwa sasa kumekuwa na changamoto mbali mbali hali inayopelekea kuyumba na maisha hususani Vijana.


"Vijana ni wazuri wapo kwenye utandawazi, dunia inaenda kasi. Ila wanatakiwa kusaidia kujitambua kwendana na utandawazi.

"Mimi naamini kwamba uwezo wa mtu ni tofauti na elimu, leo elimu inapatikana mkononi, lakini kuwa na uwezo wa kuweza yale ya nazalia, kuwa na uwezo wa kufanya yale ya kukusogeza mbele inahitaji wewe kuanza misingi yako ya maadili na uwezo mzuri ikiwemo wa kufanya kazi, kudhibiti hisia na kuwa na Maadili, lakini hii yote Kuna njia ya kupita, kama ukijitambua unaweza kudhibiti hisia na kudhibiti kukata tamaa" amesema Murtaza Adamjee.

Aidha, amebainisha kuwa, Tumaini haliwezi kuja kama hujajitambua:

"Maisha ya leo sio ya kukata tamaa, ni kuwa na tumaini na imani.





Je, unafanya matendo mema kwa namna gani, ndani yako unafanya mema kwa kwa kiasi gani lakini kwa hilo tunaendelea kujifundsha kutenda mema ndiyo inaboresha hutu na utukufu ndani yake.

"Kutenda mema ndiyo inakufungulia mengine,  

Usijiwaze wewe pekee yako Mungu anafunga njia hiyo, Kwa hiyo yale yanayofanywa hapa mfano mpango wa Good Deeds Day yanaboresha mtu wa utukufu na Imani yake na Mungu".

Aidha, amebainisha kuwa, kama unajitambua na hauishi maisha ya kuigiza, unajua kusudio lako, kwani wengine wataamini unachosema na utapata misingi imara.

"Ubongo unakusaidia na unatakiwa kuongeza uwezo wako ili Mungu akusaidie na kuwa bora  katika Dunia.

Good Deeds Day ukiwa ni mwamvuli wa harakati za kujitolea zinazolenga kuchangia maendeleo endelevu kwa kuzingatia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo uhifadhi wa mazingira, ustawi wa jamii, usawa wa kijinsia, afya bora, elimu na kupunguza umaskini, kwa lengo la kuleta matokeo chanya na kuboresha maisha ya watu kwa ujumla.

Katika kongamano hilo limewakutanisha washiriki 50 kutoka taasisi mbali mbali, likilenga kutoa muongozo, motisha na maarifa juu ya utekelezaji wa matendo mema katika jamii.



Muasisi wa Good Deeds Day Tanzania , Doroth Namuhisa


Kwa mwaka 2026, harakati za Good Deeds Day zinaongozwa na kauli mbiu “Tuungane pamoja katika kufanya matendo mema”, sambamba na maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa harakati hizo duniani, zikiwa na kauli mbiu pana zaidi ya “Tuungane kwa pamoja katika kufanya matendo mema kutoka moyoni.”

Kwa mujibu wa muasisi wa Good Deeds Day Tanzania , Doroth Namuhisa, anasema hizi ni harakati za kimataifa zinazohusisha takribani watu milioni 4.5 katika nchi 115, ambapo kila nchi kuanzia mtu binafsi, taasisi, serikali hadi mashirika wanahimizwa kushiriki kufanya matendo mema kila siku.

Imeelezwa kuwa kilele cha maadhimisho ya Good Deeds Day hufanyika kila mwaka tarehe 12 Aprili, siku inayotumika kutambua, kupongeza na kusherehekea jitihada za watu na taasisi zinazojitolea kuboresha maisha ya jamii.

Good Deeds Day ni harakati za kujitolea zinazolenga kuchangia malengo ya maendeleo endelevu, ikiwemo uhifadhi wa mazingira, ustawi wa jamii na kuleta matokeo chanya yanayoboresha maisha ya watu kwa ujumla.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI