Header Ads Widget

SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUPEWA KIPAUMBELE USHIRIKIANO WA UDSM NA CHUO KIKUU CHA VIENNA


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Vienna  katika nyanja za sayansi na teknolojia, ikiwemo nishati ya jua, ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi kwa manufaa ya pande zote mbili.

Hayo yameelezwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma) kutoka UDSM, Prof. Rose Upor alipofanya mazungumzo na  Ujumbe wa Austria ulioongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya kisiasa, Mhe. Balozi Dkt. Hannah Liko, ulipotembelea chuoni hapo  Machi 24, 2026 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu kati ya Tanzania na Austria.

Prof. Upor amesema ili kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya UDSM  na Chuo Kikuu cha Vienna, kuna umuhimu wa kuongeza ufadhili wa masomo katika kada mbalimbali pamoja na kubadilishana wataalamu watakaoweza kufundisha hata kwa njia ya mtandao. 

Naye Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Vienna, Balozi Naimi S.H. Aziz, amesema kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Austria katika sekta ya elimu una mchango mkubwa katika kukuza ujuzi, kuimarisha taasisi na kuongeza ubora wa huduma nchini.

Kwa upande wake, Dkt. Liko amepongeza ushirikiano uliopo kati ya UDSM na Chuo Kikuu cha Vienna, huku akipendekeza kuanzishwa kwa mafunzo ya lugha ya Kijerumani katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Amesema kuwa kuimarika kwa ushirikiano katika sekta ya elimu kutachangia maendeleo ya kiuchumi na kidiplomasia kwa mataifa yote mawili.

Ushirikiano kati ya UDSM na Chuo Kikuu cha Vienna unalenga maeneo manne makuu ya kimkakati, yakiwemo ubadilishanaji wa wanafunzi ili kuwapatia uzoefu wa kimataifa, ubadilishanaji wa wafanyakazi wa kitaaluma na kiutawala, utekelezaji wa tafiti za pamoja zinazogusa changamoto za kimataifa kama utawala bora na maendeleo endelevu, pamoja na uchapishaji wa kazi za pamoja za kitaaluma ili kuhakikisha mitazamo ya Afrika inawakilishwa vyema kimataifa.







 

Post a Comment

1 Comments

  1. Ningependa kumpendekeza mmoja wa wazimu wanaoheshimika zaidi wa wakati wetu. Ni mtu ambaye amewasaidia watu wengi jijini wakati wa hali ngumu.

    Baadhi ya watu hata humwita "mungu mdogo" kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiroho na jinsi anavyowasaidia wale wanaomjia kwa ajili ya mwongozo.

    Unaweza kumtumia ujumbe kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe wightmagicmaster@gmail.com

    Tafadhali zungumza naye kwa heshima na ueleze hali yako wazi, naye atajitahidi kukusaidia.

    Anatoa mwongozo wa kiroho na usaidizi kwa hali tofauti, ikiwa ni pamoja na:

    • Masuala ya mapenzi na uhusiano, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuungana tena na mpenzi wa zamani.

    • Kurejesha ndoa na mahusiano yenye matatizo.

    • Maombi na mila za kiroho kwa ajili ya ulinzi na mafanikio.

    • Tiba za mitishamba za kuponya VVU, saratani, malengelenge.

    • Maombi ya uzazi na usaidizi wa kiroho kwa wanandoa wanaotaka kupata mimba katika wiki chache.

    • Uwezo wa Telekinesis. Uwezo wa kubadilisha umbo.

    • Tambiko na maombi ya utajiri wa papo hapo.

    • Msaada wa kiroho katika hali ngumu kama vile kesi za mahakamani, kurejesha mali iliyopotea, na changamoto zingine za maisha.

    Watu wengi wamepokea msaada na mwongozo kupitia kazi yake ya kiroho.

    ReplyDelete



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI