Header Ads Widget

TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA NCHI YA MSUMBIJI



Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Msaada huo umekabidhiwa Machi 24, 2026 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na  Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá,

Akikabidhi msaada huo, Mhe. Kombo alielezea uhusiano wa karibu na wakindugu uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ulioasisiwa tokea enzi za waasisi wa mataifa hayo mawili,  Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Juliaus Kambarage Nyerere na Hayati Edward Mondlane.  Waziri Kombo alisema kufuatia udugu huo, Rais Dkt. Samia amemtuma kufikisha msaada huo ili uweze kuwapunguzia adha waathirika wa mafuriko hayo.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Rais Samia anatoa salamu za pole kwa Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo na watu wa Msumbiji kwa ujumla kutokana na madhila yaliyosababishwa na mafuriko haya na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kundelea kutoa msaada kwa  Msumbiji katika nyakati zote", Waziri Kombo alisema.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kombo alipata nafasi ya kukutana na kuzungumza na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Maria Belvinda Levy kuhusu kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, hususani kwenye masuala ya kiuchumi.

Serikali ya Msumbiji imetoa shukrani za dhati kwa kupokea  msaada huo kutoka kwa ndugu zao Watanzania ambao unabainisha taswira ya ukaribu na ushirikiano wa kweli uliopo baina ya nchi mbili hizi.



Post a Comment

1 Comments

  1. Ningependa kumpendekeza mmoja wa wazimu wanaoheshimika zaidi wa wakati wetu. Ni mtu ambaye amewasaidia watu wengi jijini wakati wa hali ngumu.

    Baadhi ya watu hata humwita "mungu mdogo" kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kiroho na jinsi anavyowasaidia wale wanaomjia kwa ajili ya mwongozo.

    Unaweza kumtumia ujumbe kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe wightmagicmaster@gmail.com

    Tafadhali zungumza naye kwa heshima na ueleze hali yako wazi, naye atajitahidi kukusaidia.

    Anatoa mwongozo wa kiroho na usaidizi kwa hali tofauti, ikiwa ni pamoja na:

    • Masuala ya mapenzi na uhusiano, ikiwa ni pamoja na kusaidia kuungana tena na mpenzi wa zamani.

    • Kurejesha ndoa na mahusiano yenye matatizo.

    • Maombi na mila za kiroho kwa ajili ya ulinzi na mafanikio.

    • Tiba za mitishamba za kuponya VVU, saratani, malengelenge.

    • Maombi ya uzazi na usaidizi wa kiroho kwa wanandoa wanaotaka kupata mimba katika wiki chache.

    • Uwezo wa Telekinesis. Uwezo wa kubadilisha umbo.

    • Tambiko na maombi ya utajiri wa papo hapo.

    • Msaada wa kiroho katika hali ngumu kama vile kesi za mahakamani, kurejesha mali iliyopotea, na changamoto zingine za maisha.

    Watu wengi wamepokea msaada na mwongozo kupitia kazi yake ya kiroho.

    ReplyDelete



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI