NA AMINA SAIDI, TANGA.
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajab Abdurahman,amewaonya wanachama wa Chama hicho kuacha mara moja tabia ya kutengeneza majungu na kampeni za mapema kuelekea uchaguzi wa ndani wa Chama hicho uliopangwa kufanyika mwaka 2027
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na viongozi wa CCM wilaya ya Tanga Rajab amesisitiza kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu katika kuwatumikia wananchi na si muda wa kupigana vita vya ndani ambavyo vinadhoofisha mshikamano.
Aidha Mwenyekiti huyo amewataka madiwani na watendaji wa Halmashauri kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ili iwe na tija,akibainisha kuwa Chama hakitavumilia kuona majengo ya miradi yakichakaa muda mfupi baada ya kukamilika kutokana na usimamizi mbovu.
"Ndugu zangu Wana CCM,huu sio wakati wa kampeni ,muda wa kampeni bado haujafika, lakini pia kuna watu ndani ya chama wanapenda kuwatengenezea wengine majungu,hivyo niwaonye waachane kabisa na tabia hiyo" Aliongeza Rajab.
"Kila mmoja wetu atekereze wajibu wake,Diwani na Halmashauri akisimama kwenye nafasi yake ni lazima maendeleo yapatikane ,huko kuna miradi mingi sana inahitaji kusimamiwa ili iwe bora,unakutana mradi umemalizika lakini baada ya muda mfupi jengo linaanza kubomoka,hii haikubaliki" Alisisitiza Rajab
Aliwataka wanachama wa Chama hicho kuachana na kampeni za mapema kabla ya 2027 ,
" Kila mwanachama ,ahakikishe anajiepusha na kampeni za mapema kabla ya muda wa uchaguzi wa Chama cheti 2027,kuna watu wameanza kupita pita huko mtaani na wengine wanapiga majungu ya kuchafuana ,hii haikubaliki kabisa kwenye chama cheti,kila mmoja wetu ajiepushe na kampeni za mapema na tufuate utaratibu wa Chama cheti"Aliongeza Rajab
MWISHO







0 Comments