Rais wa Urusi Vladimir Putin amempongeza Mojtaba Khamenei kwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Iran na kusisitiza uungaji mkono wa Moscow kwa Tehran.
"Naomba upokee pongezi zangu za dhati kwa kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran," Putin anasema katika ujumbe uliochapishwa kwenye tovuti ya Kremlin.
Kiongozi huyo wa Urusi pia anasema "anathibitisha tena uungaji mkono [wa Urusi] usioyumba kwa Tehran na mshikamano na marafiki zetu wa Iran" na kuahidi kuwa "atasalia mshirika anayetegemewa".
"Wakati ambapo Iran inakabiliana na mashambulizi, hatua zako katika nafasi hii ya juu bila shaka zitahitaji ujasiri mkubwa na kujitolea. Nina imani kwamba utaendeleza kwa heshima kazi ya baba yako na kuwaunganisha watu wa Iran katika kukabiliana na majaribu haya makubwa," anasema.





0 Comments