Header Ads Widget

WACHEZAJI 23 WAPEWA KADI NYEKUNDU BAADA YA RABSHA KUZUKA BRAZIL

 

Mshambuliaji wa zamani wa Brazil na FC Porto Hulk alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopewa kadi nyekundu
Wachezaji 23 wamepewa kadi nyekundu baada ya vurugu kubwa kuzuka kati ya vilabu vya Brazil Cruzeiro na Atletico Mineiro wakati wa fainali ya Campeonato Mineiro.

Kaio Jorge alifunga bao la ushindi huko Belo Horizonte huku Cruzeiro, inayonolewa na kocha wa zamani wa Brazil, Tite, ilipowalaza wapinzani wao Atletico 1-0 na kuwa mabingwa wa jimbo la Minas Gerais kwa mara ya kwanza tangu 2019.

Lakini mechi hiyo ilikumbwa na vurumai kali ndani ya sekunde hizo, hali iliyowalazimu maafisa wa usalama na polisi wa kijeshi kuingilia kati na kusababisha wachezaji 23, akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Atletico wa Brazil, Hulk, kutolewa uwanjani kwa kadi nyekundu.

Makabiliano hayo makubwa yalianza pale kipa wa Atletico, Everson, alipomsukuma Christian na kumuangusha chini, kuweka goti lake kwenye kifua cha kiungo huyo wa Cruzeiro, ambaye aligongana naye wakati akifukuzia mpira.

Wenzake Christian mara moja walikabiliana na Everson, na kumsukuma kipa kwenye nguzo ya goli, jambo lililozua maswali huku wachezaji wengi wakijiunga na vurumai hilo, wafanyakazi wa usalama wakijaribu kutenganisha timu hizo.

Ingawa hakuna kadi nyekundu iliyotolewa na mwamuzi Matheus Delgado Candancan wakati wa mchezo, chombo cha habari cha Brazil Globo kiliripoti, wachezaji 23 walitolewa nje baadaye kwa sababu pambano lilimzuia afisa wa mechi kuonyesha kadi uwanjani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI