Header Ads Widget

PPP NJIA YA KUIMARISHA SEKTA BINAFSI NA KUPAISHA UCHUMI WA TANZANIA KUFIKIA TRILIONI


Dar es Salaam 

Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPP unaendelea kuwa chachu ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini, kwa kuunganisha rasilimali, utaalamu na uwekezaji wa sekta binafsi ili kupandisha uchumi wa taifa hadi kufikia thamani ya trilioni.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi PPPC, David Kafulila katika kongamano la lililoandaliwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) Aprili 09, 2026 amesema, jukumu la taasisi hiyo ni kuratibu ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha miradi inayofaa kutekelezwa kwa mfumo wa ubia inasimamiwa kwa ufanisi. 

“Lengo letu ni kuhakikisha miradi ya PPP inatekelezwa kwa ufanisi huku tukiwashirikisha wadau wote katika maendeleo ya uchumi,” amesema.




Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema sekta binafsi inatarajiwa kuchangia takribani asilimia 70 ya fedha za Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Miaka Mitano kupitia uwekezaji na miradi ya ubia, mpango unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Naye Mwanahamisi Singano, Mkurugenzi wa Sera na Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, baadhi ya wadau wamesema ni muhimu kuanzisha mfumo wa one stop center, kuundwa kwa bodi ya maendeleo, kutoa mafunzo maalum kwa wataalamu wa PPP, kufanya tafiti za kina  kabla ya utekelezaji na kuhakikisha kunakuwa na ujumuishi wa wadau wote.

Aidha Singano amesisitiza kuwa changamoto ya kucheleweshwa kwa malipo kwa sekta binafsi, ambayo mara nyingine husababisha baadhi ya kampuni kufilisiwa na taasisi za fedha, lazima kushughulikiwe ili miradi iendelee kwa ufanisi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI