Na,Jusline Marco;Arusha
Katika kuadhimisha siki ya wanawake Duniani Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imetoa pongezi kwa Afisa Uhifadhi Mkuu daraja la 1 Lohi Zakaria kwa kuwa na uzoefu wenye Maarifa katika utendaji kazi ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
Katika utekelezaji wa majukumu yake kwa miaka 34 alijulikana kwa jina la Utani Profesa kutokana na uwezo mkubwa wa kujua vitu vingi katika hifadhi ya Ngorongoro.
Ofisi ya NCAA imemuelezea Afisa Lohi kuwa mwanamke shupavu hivyo kuelekea siku ya wanawake Duniani itakayoadhimishwa tarehe 8 Machi mwaka huu, NCAA inamvika Pete anapotimiza miaka 6 ya tukio la Faru.
Tukio la kusisimua na hatari katika maisha yake la tarehe 6 Machi 2020 katika Kreta ya Ngorongoro kwenye utekelezaji wa majukumu yake, alitokea Faru na kumkimbiza bila yeye kujua ambapo alijaribu kutumia mbinu za medani alizofundishwa jeshini kujinasua lakini bahati mbaya alishambuliwa ingawa baadaye aliweza kuokolewa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
Kamanda huyu wa Uhifadhi anaadhimisha siku ya wanawake duniani akiendelea kuchapa kazi na mara nyingi utamkuta kreta akifanya shughuli za uhifadhi, utafiti, sensa za wanyamapori na kupambana na mimea vamizi bila woga.






0 Comments