Katika kuadhimisha Siku ya Wanyamapori Duniani na kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), kupitia Kanda ya Kati imetoa elimu ya uhifadhi pamoja na kufadhili mahitaji mbalimbali kwa Shule za Sekondari Sanza na Nkonko zilizopo katika Mkoa wa Singida.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vifaa vya kujifunzia, vifaa vya usafi pamoja na kiti mwendo.
Zoezi la utoaji wa vifaa hivyo liliambatana na upandaji wa miche ya miti zaidi ya 100.









0 Comments