Header Ads Widget

MKUTANO MKUU DOREFA WAPITISHA MPANGO KAZI WA MWAKA 2026-2027


Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima media Dodoma


WAJUMBE  wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) wamepitisha  Mpango kazi wa mwaka 2025-2026 wa Chama cha Soka Mkoani Dodoma.

Awali kabla ya kuupitisha Mpango kazi huo,wajumbe hao walisomewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma CPA,Edwin Michael na kisha kwa kauli moja kuupitisha katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama hicho uliofanyika leo Machi 28,2026 Jijini Dodoma.

Moja ya malengo ni kuhakikisha kunakuwa na ligi imara na yenye ushindani kwa vijana,kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake pamoja na kuendeleza ushirikiano na wadau wa Soka.

"Mpango kazi huu,wa mwaka 2026-2027 unaweka msingi imara wa Maendeleo ya mpira wa miguu Mkoa wa Dodoma Kwa kushirikiana na wadau wote wa michezo na kuhakikisha Mkoa unakuwa na ushindani wa Kitaifa na Kimataifa,"amesema CPA Michael.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI