Na Catherin Kilwale (UoI)Matukio Daima Media
Msitu wa Nyumbanitu ni msitu wa asili wenye thamani kubwa ya kijamii, kihistoria na kiutalii uliopo kijijini Mlevela, Kata ya Mdandu, Wilaya ya Wanging’ombe katika mkoa wa Njombe, Tanzania. Msitu huu unakaribia kilomita 15‑20 kutoka Njombe Mjini.
Pia jina Nyumbanitu linatokana na usemi wa Kiwabena uliomaanisha “nyumba nyeusi”, kutokana na kuwepo kwa mapango na mapango ya mawe ndani ya msitu ambayo ni giza na mazito kuona ndani yao,Mapango haya yalikuwa makazi ya watu wa zamani na pia kutumika wakati wa vita.
Msitu wa Nyumbanitu umecheza nafasi muhimu katika historia ya jamii za hapa Tanzania kwani mapango makubwa ndani ya msitu yalitumika kama sehemu ya kujificha wakati wa vita kati ya makabila ya Wabena na Wahehe karne ya 19 yalihifadhi watu dhidi ya vikosi vya Kijerumani wakati wa Maji Maji Uprising (1905–1906).
Licha ya hivyo kuna utamaduni wa Kiasili ambao Wabena wanaendelea kutumia eneo hili kwa matambiko ya jadi, ibada na mila zao za kihistoria, Msitu huu ni kitovu muhimu cha urithi wa jamii hii na nyanda za juu kusini kwa sababu ni mahalipanapo tunzaa simulizi za mababu zetu.
Katika msitu huu kuna ‘kuku weusi’ ambao huonekana mara kwa mara ndani ya msitu wanaojulikana kama wanyama wa ajabu ambao hawafugwi na mtu, na wengi wanaamini ni wa kipekee kutokana na maajabu walio nayoo,
Msitu huu unavutia watalii kwa sababu ya mchanganyiko wa asili, historia na utamaduni kwani watu wengii hufika eneohiloo kwaajili ya kushangaa maajabu mkubwa ya msitu huu wageni na wenyeji hufurahishwa na matukio ya ajabu yanayo patikana katika msitu huu.
Msitu wa Nyumbanitu umepewa umuhimu rasmi na Wizara ya Mali Asili na Utalii ya Tanzania kama kivutio muhimu cha utalii na utamaduni, na jamii za wenyeji zimeelekezwa kuendelea kuutunza msitu huu kwa heshima ya urithi na historia yake.

.jpg)




0 Comments