NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MWANZA.
MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Jubilate Lauwo, amesema amani, utulivu na usalama ni mambo muhimu yatakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za uzalishaji na kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.
Lauwo ameyasema hayo leo Oktoba 1, 2026 wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Amina Makilagi, ambaye amehamishiwa Wilaya ya Magu.
Amesema Nyamagana ina wananchi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji, hivyo ni muhimu kuweka mazingira yatakayowezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa amani na usalama.
Amesema katika kipindi chake cha uongozi atashirikiana na Kamati ya Usalama pamoja na watumishi wengine kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwepo katika wilaya hiyo.
“Nitashirikiana vema na Kamati ya Usalama ili wananchi wetu wazidi kufanya shughuli zao za uzalishaji vizuri,” amesema Lauwo.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesema katika utekelezaji wa majukumu yake atazingatia kauli mbiu ya “Tushirikiane, tusikilize wananchi, tulinde amani ya Nyamagana tuweke maendeleo ya wananyamagana mbele" Alisema Lauwo.
Akikabidhi ofisi aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amemshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania dkt Samia suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumteua kuwa mkuu wa Wilaya ya Magu.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine, amesema ana imani na Mkuu huyo wa Wilaya kutokana na utendaji wake na kuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.










0 Comments