Header Ads Widget

DESTINATION NGORONGORO YADHIHIRISHA BINADAMU HAKUWA NYANI



Washiriki wanaohudhuria mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Elimu kwa Umma unaoandaliwa na shirika la  Utangazaji Tanzania (TBC) wamepigwa msasa kuhusu maajabu ya Ngorongoro  na kuelezwa ukweli kuhusu masalia ya binadamu wa kale yanayopatikana ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Akitoa mada kuhusu hifadhi ya Ngorongoro Afisa Utalii Msaidizi Bw. Hillary Remen ameeleza washiriki hao kuwa Ngorongoro ni hifadhi yenye  maajabu na ina uthibitisho usiotiliwa shaka kuhusu ushahidi wa binadamu wa kale aliyetembea wima kwa miguu miwili kupatikana ndani ya hifadhi hiyo.

Pamoja na ukweli kuhusu historia ya binadamu, Ngorongoro ina maajabu mengi na vivutio vingi  vinavyojumuisha Kasoko ya Ngorongoro (Bustani ya Edeni), Nyayo za Laetoli kama ushahidi wa hatua za kwanza za binadamu kutembea wima, Bonde la Olduvai  lenye ushahidi wa chimbuko la binadamu na masalia ya wanyama wa kale, Tamaduni hai,  mazalia ya Nyumbu katika eneo la Ndutu, misitu, maporomoko ya maji na kreta 3 za kipekee. 

Historia ya binadamu wa kale kutembea kwa miguu miwili imebainishwa kwa ufasaha kupitia Urithi Geopark Museum iliyopo wilayani Karatu. Historia hiyo inabainisha wazi kuwa binadamu wa kale alibadilika kutokana na mazingira na nyakati ila  miongo yote binadamu amebaki kuwa binadamu.

Mkutano wa Washitiri unafanyika Jijini Arusha kwa wiki moja na unatarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambapo Ngorongoro inashiriki mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI