Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Wananchi wa kata za Ikondo,Nshamba na Muleba wilayani Muleba mkoani Kagera wanatarajia kujua kwa uchumi wap kufuata kukamilika kwa daraja la Kamishango ambalo ni kiunganishi muhimu kwa kata hizo katika kusafirisha bidhaa zao ikiwemo ndizi.
Akizungumza wakati wa ziara ya Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa, Ndug.Kenani Kihongosi, meneja wa wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Kagera mhandisi Samwel Mwambungu ameeleza kuwa kwa sasa daraja hilo limekamilika kwa asilimia mia moja na kukamilika kwa daraja hilo litachochea uchumi wa kata hizo na wilaya ya Muleba kwa ujumla.
"ujenzi la daraja hilo umekamilika kwa asilimia mia moja ukiacha shughuli ndogo zilizo bakia ni pamoja na usimikaji wa taa 56, upakaji rangi wa kingo za daraja pamoja usafishaji wa eneo ili daraja lianze kutumika ambapo kukamilika kwa daraja hili itachichea uchumi na kuongeza mnyororo wa thamani kwa wilaya ya Muleba"
Aidha Mhandisi Mwambugu ameeleza kuwa mradi huo uneghalimu kiasi cha shilingi bilioni 12.5 na kutekelezwa na mkandarasi mzawa DRK General Merchants Ltd, likiwa na urefu wa kilometa 45 na maungio ya barabara ya kilometa 2.
"mradi huu ulianza kutekelezwa kuanzia mwezi November mwaka 24, kwa gharama ya shilingi billioni 12.5 likihusisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 45 maungio ya barabara yenye urefu wa kilometa 2"
Kwa upande wake Kenani Kihongosi amesema amempongeza mkandarasi aliyekeleza ujenzi wa daraja hilo pamoja na usimamizi mzuri wa TANROADS mkoa wa Kagera, na kumshauri mkandarasi kumalizi kazi ndogo zilizosalia ili daraja hilo lifunguliwe na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ili kukuza uchumi wao.
"nilipofika hapa nilikuwa najiuliiza hiki ni kitu gani ni maeneo machache inatekelezwa miradi mikubwa kama hii ya shilingi billioni 12.5, nimpongeze mkandarasi na pia TANROADS mkoa wa Kagera, ninachomtaka mkandarasi ni kumalizia mradi kwa wakati ili kuruhusu wananchi kupata huduma"
Aidha katika hatua nyingine mwenezi huyo wa CCM taifa, amesema kuwa daraja hilo ni muhimu katika kukuza uchumi wananchi na taifa kwa ujumla na kuokoa maisha ya wananchi ambapo pia amewataka wananchi kulitunza daraja hilo ili lidumu kwa muda mrefu.
Nao baadhi ya wananchi, akiwemo Bi Spenzioza Protazi na Bw. Abdurashid Yunusu, wameipongeza serikali kwa kutekeleza mradi huo, wakisema kuwa hapo awali walikumbwa na changamoto ya magari kukwama katika eneo hilo pamoja na kujaa maji wakati wa mvua kutokana na udogo wa daraja la zamani.
Daraja la Kamishango ni miongoni mwa madaraja matano yanayotekelezwa mkoani Kagera kwa gharama zaidi ya shilingi billioni 45.6, kufuatia mvua za El nino zilizonyesha mwaka 2023 katika maeneo mengi hapa nchini na kusababisha uharibifu wa miundombinu.



.jpg)







0 Comments