Header Ads Widget

BILIONI 64 ZAKARABATI UWANJA WA NDEGE IRINGA


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP 

IRINGA.Ili kukuza uchumi na kuboresha shughuli za utalii katika hifadhi zilizopo mkoani Iringa,Kiasi Cha shilingi bilioni 64 kimetumika kuboresha miundombini katika uwanja wa ndege Kwa ajili ya wasafari wa anga.

‎‎Mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James  wakati akifungua kongamano la wadau wa habari /Wahariri na Waandishi wa habari kusini mwa Tanzania  MISA TAN SUMMIT amesema maboresho hayo yamelenga kuhakikisha wasafiri wa anga na watalii wanatumia uwanja huo vizuri na sasa safari za ndege zinapatikana siku zote za wiki.

‎‎Pia mkuu huyo wa mkoa amesema Kwa sasa, Serikali inaendelea na ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja huo pamoja na eneo la maegesho ya magari, unaogharimu takribani Shilingi bilioni 41.06 ambapo jengo hilo linatarajiwa kuhudumia abiria takribani 120 kwa wakati mmoja.

Aidha James amesema kufanyika kwa kongamano Hilo kubwa la wanahabari mkoani Iringa kunapaswa kutumika katika kutangaza fursa zilizopo ili Jamii na Taifa liweze kunufaika.

‎‎Hata hivyo Amesema asilimia 82 ya ajira kwa wakazi wa Iringa  zimetokana na shughuli za kilimo na hivyo ni ajenda muhimu za kufanyia kazi kupitia vyombo vya habari.

‎Awali Mwenyekiti wa MisaTanzania Edwin Soko ameahidi kufanyia kazi kupitia wanahabari waliopo fursa na utalii uliopo mkoani Iringa ili Jamii iweze kuzitumia.

‎‎Mkuu wa wilaya ya Iringa Benjamin Sitta amewataka wanachama wa MisaTanzania ambao ni wanahabari kuhakikisha wanapeleka ujumbe kwa Jamii namna ya kuziendea na kuzitumia fursa zilizopo nchini ili kuondokana na wimbi la umasikini. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI