Header Ads Widget

BALOZI SIRRO ATAKA UMEME WA UHAKIKA KUKUZA UCHUMI KIGOMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amelitaka Shirika la Uzalishasema na ugavi wa umeme (TANESCO) mkoa Kigoa kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana mkoani humo ili utafsiri kwa vitendo mpango mkakati wa serikali wa kuufanya mkoa huo kitovu cha uchumi na biashara kwa ajili ya soko la nchii za ukanda wa maziwa makuu.

Balozi Sirro alisema hayo akikabidhi magari matano, bajaji tatu na pikipiki nne kwa uongozi wa Shirika la Uzalishaji na ugavi wa umeme (TANESCO) mkoa Kigoma ambapo alisema kuwa umeme wa uhakika  ni kichocheo  cha utekelezaji uzalishaji na wenye tija wa shughuli za biashara na uchumi mkoani humo.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma,DkRashid Chuachua alisema kuwa kwa miaka mingi umeme ulikuwa kikwazo kwa maendeleo ya kiuchumi ya mkoa huo hasa suala la viwanda na kwamba kuna watu wengi walitamani kuwekeza kwenye viwanda Kigoma wakawa wanaogopa lakini kwa sasa kumekuwa na idadi kubwa ya wawekezaji waliojitokeza wanaotaka kuwekeza kwenye Nyanja mbalimbali mkoani Kigoma.


Akizungumza katika makabidhiano hayo Kaimu Meneja wa TANESCO mkoa Kigoma,Hassan Nganjau alisema kuwa kupokewa kwa magari, bajaji na pikipiki  hizo ni jambo kubwa kwa TANESCO Kigoma na wilaya zake kwani zitasaidia kuchochea utendaji kazi katika kupeleka umeme kwa wateja mbalimbali hasa wakati huu ambapo mkoa  wamekuwa na idadi kubwa ya wateja wanaotaka kuunganishwa kwenye umeme baada mkoa kuungwa kwenye gridi ya Taifa.

                             Hassan Nganjau   Kaimu Meneja wa TANESCO mkoa Kigoma

Kwa upande wake Meneja wa TANESC wilaya ya Kakonko, Mese Mwanga alisema kuwa kwenye miradi ya Umeme Vijijini chini ya REA kumekuwa na idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji umeme hivyo kuwepo kwa magari hayo kwao kutasadia kusimamia miradi mbalimbali iliyopo kwenye maeneo yao na kusaidia kupatikana kwa umeme wa uhakika wakati wote.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI