Header Ads Widget

TPDA YATOA TAARIFA MSIBA WA DJ WA KWANZA NCHINI FRANSIS BUNDALA, KUZIKWA LEO JIONI MAKABURI YA KINONDONI

 

Marehemu Fransis Bundala (Dj Sweet Fransis)

Na. Matukio Daima Media, Dar.


MAZISHI ya Manju wa muziki DJ wa kwanza Nchini Fransis Bundala (Dj Sweet Fransis) ambaye ndiye alikuwa Dj wa kwanza kufanya shughuli hiyo ya kuchezesha muziki hapa nchini atazikwa leo February 16, 2026 saa 10:00 kwenye Makabuli ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma iliyotolewa na Tanzania Professional DJs Association (TPDA) kupitia kwa Katibu Mkuu wake Asanterabbi Mtaki amebainisha kuwa, ibada ya kuuaga mwili wa marehemu itaanza saa saa 7 mchana kwenye hospital ya Mwananyamala ambapo marehemu ndipo alipokuwa akipata matibabu na kufariki siku ya jumamosi saa 1:00 Usiku l.

Ambapo imeongeza kuwa: Marehemu Dj Sweet Fransic ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 71 alikuwa anasumbuliwa na Moyo kuwa Mkubwa na Mapafu kutofanya kazi vizuri.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI