Header Ads Widget

TANZANIA YANADI VIVUTIO VYA UTALII KATIKA ONESHO LA OTM NCHINI INDIA

 


Tanzania imeendelea kunadi vivutio vya utalii, mazao ya utalii na fursa za uwekezaji  zinazopatikana nchini Tanzania katika onesho la Kimataifa la Utalii - OTM ( Outbound Travel Mart) linaloendelea, jijini Mumbai nchini India, ambalo limeanza  rasmi tarehe 05  Februari,2026 na kuhitimishwa  leo Februari 07, 2026.

Onesho la  OTM  ni jukwaa muhimu kimataifa katika  kutangaza, kuendeleza na kukuza biashara za utalii duniani.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki  onesho hili adhimu linalokutanisha wadau  wakubwa wa utalii  duniani na kuendelea  kuonesha vivutio vya kipekee vya utalii vikiwemo wanyamapori, mandhari, fukwe, malikale na utamaduni sambamba na kuhamasisha fursa mbalimbali za uwekezaji  zinazopatikana katika  Hifadhi za Taifa ishirini na moja (21) zilizopo Tanzania.

Aidha, TANAPA inatumia jukwaa hili adhimu la  onesho la  OTM, kuendeleza mikakati ya nchi ya kujitangaza  na kuongeza  mashirikiano katika masoko ya utalii duniani. Hatua hii  ni mkakati mahususi katika kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa hususani soko la India  wanaotembelea Hifadhi za Taifa Tanzania pamoja na kukuza pato la utalii na kuchangia kwa kiwango kikubwa   uhifadhi na uchumi endelevu wa taifa kwa ujumla.

Ushiriki wa TANAPA katika onesho hili  ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvutia masoko mapya ya watalii, na kuendeleza utalii endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI